Institute of Languages (INSTL)

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 5 of 7
  • Item
    Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.
    (Kabale University, 2022) Masika, Doreen
    Mradi huu wa tamthilia umepewa anwani ya " kiza cha mchana " kimaksudi. K wa kawaida kiza hujitokeza wakati wa usiku lakini siyo wakati wa mchana kwa hivyo kiza kikijitokeza mchana kuna maana kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa. Mtu yeyote azaliwapo huwa anatarajia mema na ufanisi katika maisha yake lakini baadhi ya watu duniani na katika nchi hii, matarajio yao hugeuka ndoto ya mchana yaani huishia yakiwa kinyume kabisa na matarajio ya watu hawa. Mradi wa tamthilia ya "kiza cha mchana" utadhihirisha wazi wazi jinsi baadhi ya watu wanakumbana na matatizo chungu nzima; tatizo baada yajingine mpaka wanapoanza kujichukia na kulaani siku walizozaliwa. Tamthilia hii itamtia mtu moyo ambaye anakumbana na matatizo katika maisha yake kwamba matatizo ni sehemu ya maisha ya binadamu na sio mwisho wa maisha ya binadamu, wakiyavumilia wakaendelea kujitahidi kadri ya uwezo wao huku wakimwomba Rabana, mwishowe watafanikiwa na hali yao kubadilika kabisa na kuanza kuishi kwa raha mustarehe. Mhusika mkuu, Matatizo ambaye ni fakiri atakumbana na matatizo mengi; moja baada ya jingine licha ya kuwa mchochole wa kupigiwa mfano. Matatizo analemewa na kuanza kujichukia na mwishowe anaokoka na baada ya muda mfupi anafanikiwa na kutajirika kutokana na bahati asiyoilalia wala kuiamkia. Watu kama hawa huishia kwa kujitia kitanzi baada ya kukumbana na mfululizo wa matatizo kama njia ya kuondokea matatizo haya na kuiacha familia yao katika dhiki kubwa. Kwa hivyo, mradi huu unapinga kabisa kuj itia kitanzi kama suluhisho la mfululizo wa matatizo bali kuwatia moyo na kuendelea kufukuza ndoto zao huku wakiimezea mate machungu hali yoyote ile wanayokumbana nayo mpaka watakapofaulu. Matatizo hapa amechorwa kama maskini, mvumilivu, ili kuwapa watu kama hawa mfano mzuri. Mradi wa tamthilia utapangwa katika vitendo vitatu na kila kitendo kitakuwa na maonyesho matatu. Kila kitendo kitakuwa na maudhui kuu linalozungumziwa humo ambalo linajitosheleza. Kila onyesho litakuwa na maudhui kuu pamoja na maudhui mengine madogo. Maudhui haya ya vitendo na maonyesho yatachangiana na kukamilishana na kufanya tamthilia nzima yenye wazo kuu la matatizo yaani anwani yenyewe ya mradi. Maudhui yatakayoshughulikiwa yatakuwa miongoni mwa utabaka, matatizo, uasherati, migogoro ya kifamilia, uvumilivu, ukengeushi, unafiki, mabadiliko, dini, baraka. vi Msanii wa mradi atatumia wahusika mbalimbali ambao ni pamoja na wahusika wakuu, wahusika wadogo, wahusika bapa, wahusika mviringo na wahusika wa kisaikolojia. Wahusika hawa watakuwa na mienendo ambayo ni pamoja na wavumilivu, wajibikaji, waaminifu, wakengeushi, washerati, wapole, werevu masomoni, washauri wema. Wahusika wakuu ndio watakaosheheni ujumbe muhimu na wahusika wadogo watawasaidia wahusika wakuu kukamilisha dhamira na maudhui ya msanii. Mazungumzo yataendelezwa miongoni mwa wahusika hawa ambapo nafsi ya kwanza umoja (ni ) na wingi ( tu ) zitatumika hasa kuendeleza mazungumzo baina ya wahusika. Nyimbo, majazi, taswira navyo vitatumika kuwasilisha ujumbe. Wahusika hawa watakuwa na maleba ambayo yataambatana sambamba na mandhari husika na wazo litakalokuwa likiendelezwa na wahusika hawa. Maleba yatakayotumiwa yatakuwa pamoja na magwanda, majoho ya kitabibu, majoho ya mapadre, ndala, veli. Maelekezo ya jukwaa yatatumiwa ipasavyo iii kuwaielekeza hadhira kutambua kwa urahisi maleba, miondoko na maingio ya wahusika na sifa zao. Maelekezo ya jukwaa yataandikwa kwa hati za mkazo na kuwekwa katika mabano. Maelekezo ya jukwaa haya pia yataonyesha wakati na mandhari ambapo vitushi vitatendeka. Mandhari haya yatakuwa pamoja na nyumbani, shambani, zahanatini. hospitalini kanisani.
  • Item
    Mradi wa Kutunga Tamthilia ya "Mama Mkwe’’.
    (Kabale University, 2022) Tusasibwe, Bosco
    Kudhihirisha ubunifu wa kazi za fasihi unaotokana na umilisi wa ujifunzaji wa fasihi bunilizi ya Kiswahili, Kuchangia idadi ya Tamthilia za Kiswahili ambazo zimeandikwa katika mazingira ya Uganda kwa ajili ya kukuza na kuendeleza ujifunzaji, ufundishaji na usomaji wa kazi za fasihi ya Kiswahili Uganda, Kueleza maswala ya kimaisha ya binadamu katika mazingira yake, changamoto na ukombozi wake wa kujenga maisha bora
  • Item
    Dhima ya Methali Ktika Ukuzaji wa Nidhamu Baina ya Wanajamii Kijijini Bungandaro, Wila Yani Rubanda Nchini Uganda.
    (Kabale University, 2022) Atwiniramasiko, Ivan
    Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza dhirna ya methali katika ukuzaji wa nidhamu baina ya wanajamii kijijini Bungandaro, wilayani Rubanda nchini Uganda. Dhima za methali katika ukuzaji wa nidhamu zilichunguzwa katika utafiti huu. Aidha utafiti huu umeziainisha methali katika makundi matatu makuu, yaani uainishaji huu hutegemea rnaana ya ndani pamoja na maana ya nje na walengwa wa rnethali husika. Vile vile, methali zirneainishwa kulingana na maudhui ya kimsingi yanayowasilishwa ndani ya methali hiyo hiyo, pamoja na uainisho wa kimafunzo. Makundi hayo ni pamoja na: Methali za kukashifu tabia mbaya miongoni mwa wanajamii, Methali za kuhimiza heshima kwa wazima miongoni mwa wanajamii pamoja na Methali za kuleta amani miongoni mwa wanajamii. Basi, makundi haya yote hukuza na kutimiza swala la nidhamu baina ya wanajamii. Utafiti huu umeundwa na sura tano yaani sura ya kwanza, pili, tatu, nne na tano. Sura ya Kwanza imeshughulikia Utangulizi, Tatizo la utafiti, Malengo ya Utafiti, Upeo wa utafiti, Umuhimu wa Utafiti na Changamoto zilizoukabili utafiti huu. Sura ya Pili imeshughulikia Mapitio ya Kitaaluma na ya Kazi tangulizi ambapo imeelezea yaliyoandikwa kuhusu methali na jinsi zinavyoweza kukuza nidhamu baina ya wanajamii. Aidha, imeelezea yaliyoandikwa kuhusu makundi pamoja na uanisho wa methali katika hali au masuala tofauti tofauti. Kadhalika, sura ya pili irneelezea Pengo la Maarifa na Kiunzi cha utafiti wa awali pamoja na jinsi utafiti huu ulivyoziba kiunzi au pengo li'ilo. Sura ya Tatu irnezungumzia Njia na Mbinu za Uafiti. Imezungumzia Utangulizi, Eneo la Utafiti, Sampuli ya Utafiti na Usampulishaji, Ukusanyaji wa Data. Uchambuzi wa Data na Vifaa vya Utafiti.Sura ya Nne imeeleza juu ya Uwasilishaji na Uchambuzi wa data,ambapo imeelezea aina za teknolojia ambazo huwa na dhima katika ukuzaji wa nidhamu. Sura ya tano imeeleza juu ya Muhtasari wa Utafiti na Mapendekezo.
  • Item
    Athari za Runyankole-Rukiga Katika Uandishi wa Insha Za Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili wila yani Kabale.
    (Kabale University, 2021) Musiimenta, Donath
    Kutambua athari za Runyankole- Rukiiga kwenye uandishi wa insha za Kiswahili miongoni mwa wanafunzi, Kueleza athari zinazojitokeza katika uandishi wa insha za Kiswahili miongoni mwa wanafunzi, Kuelezavyanzo vya athari katika uandishi wa insha na wanafunzi. Utafiti huu ulikuwa unawalenga wanafunzi wa kidato cha nne na sita ambao wanashughulikia uandishi wa insha na walimu wao watatu. Mtafiti alimhoji kila mwanafunzi ambapo moja wao walijua Kiswahili ipasavyo kilichomletea kupata data chache.
  • Item
    Athari Ya Maumbo Ya Lugha Ya Kiswahili Katika Msamia Ti Wa Lugha Ya Lufumbira.
    (2021) Sunday, Emmanuel
    Uchunguzi huu ulihusu athari za maumbo ya lugha ya Kiswahili kwa msamiati wa Lufumbila nchini Uganda tukilenga wilaya ya Kisoro. Uliendeana na maakisio ya malengo mawili muhimu yaliyoungoza tangu mwanzo hadi mwisho. Lengo kuu la uchunguzi huu lilikuwa ni kubainisha athari za maumbo ya Kiswahili katika msamiati wa Lufumbila. Hata hivyo, malengo mahususi ya uchunguzi huu, yalikuwa ni pamoja na Kutambua jinsi athari za maumbo ya zinazvyojitokeza baina ya Kiswahili na Lufumbira, lengo la pili lilikuwa ni Kubainisha njia za kukabiliana na athari za Kiswahili katika msamiati wa Lufumbila. Utafiti huu ulitumia mbinu ya hojaji, matumizi ya maktaba pamoja na mahojiano. Hojaji ilitumiwa kwa kuandika maswali kwenye makaratasi na kuyapelekeya watafitiwa. Matumizi ya maitaba ni mbinu nyingine iliyotumiwa katik kukusanya data, makala ya watafiti wa awali yalisomwa moja kwa moja kwa kulingana namalengo ya utafiti. Mbinu nyingine ni mahojiano, pia katika utafiti huu tulitumia mazungumzo ya ana kwa ana huku tukifanya maakisio na malengo ya utafiti huu. Keywords: Athari, Maumbo, Lugha, Kiswahili Katika Msamia Ti, Lugha, Lufumbira.