Dhia Ya Methali Ktika Ukuza.Ji Wa Nidhamu Baina Ya W Anajamii Kijijini BungandaroWilayanirubanda Nchini Uganda.

Loading...
Thumbnail Image

Date

2021

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Kabale University

Abstract

Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza dhima ya methali katika ukuzaji wa nidhamu baina ya wanajamii kijijini Bungandaro, wilayani Rubanda nchini Uganda. Dhima za methal i katika ukuzaji wa nidhamu zilichunguzwa katika utafiti huu. Aid ha utafiti huu umeziainisha methali katika makundi matatu makuu, yaani uainishaji huu hutegemea maana ya ndani pamoja na maana ya nje na walengwa wa methali husika. Vile vile, methali zimeainishwa kulingana na maudhui ya kirnsingi yanayowasilishwa ndani ya methali hiyo hiyo, pamoja na uainisho wa kimafunzo. Makundi hayo ni pamoja na: Methali za kukashifu tabia mbaya miongoni mwa wanajamii, Methali za kuhimiza heshima kwa wazima miongoni mwa wanajamii pamoja na Methali za kuleta amani miongoni mwa wanajamii. Basi, makundi haya yote hukuza na kutimiza swala la nidhamu baina ya wanajamii. Utafiti huu umeundwa na sura tano yaani sura ya kwanza, pili, tatu, nne na tano. Sura ya Kwanza imeshughulikia Utangulizi, Tatizo la utafiti, Malengo ya Utafiti, Upeo wa utafiti, Umuhimu wa Utafiti na Changamoto zilizoukabili utafiti huu. Sura ya Pili imeshughulikia Mapitio ya Kitaaluma na ya Kazi tangulizi ambapo imeelezea yaliyoandikwa kuhusu methali na jinsi zinavyoweza kukuza nidhamu baina ya wanajamii. Aidha, imeelezea yaliyoandikwa kuhusu makundi parnoja na uanisho wa methali katika hali au masuala tofauti tofauti. Kadhalika, sura ya pili imeelezea Pengo la Maarifa na Kiunzi cha utafiti wa awali pamoja na jinsi utafiti huu ulivyoziba kiunzi au pengo fiilo. Sura ya Tatu imezungumzia Njia na Mbinu za Utafiti. Imezungumzia Utangulizi, Eneo la Utafiti, Sampuli ya Utafiti na Usampulishaji, Ukusanyaji wa Data. Uchambuzi wa Data na Vifaa vya Utafiti.Sura ya Nne imeeleza juu ya Uwasilishaji na Uchambuzi wa data,ambapo imeelezea aina za teknolojia ambazo huwa na dhima katika ukuzaji wa nidhamu. Sura ya tano imeeleza juu ya Muhtasari wa Utafiti na Mapendekezo.

Description

Keywords

Dhia, Methali, Ukuza, Nidhamu Baina, Anajamii, BungandaroWilayanirubanda, Uganda

Citation

Atwinlramasiko, Ivan (2021). Dhia Ya Methali Ktika Ukuza.Ji Wa Nidhamu Baina Ya W Anajamii Kijijini BungandaroWilayanirubanda Nchini Uganda. Kabale: Kabale University.