Kabale University Digital Repository (KAB-DR)

KAB-DR preserves research output from the Kabale University community

 

Communities in KAB-DR

Select a community to browse its collections.

Now showing 1 - 4 of 4
  • The collections in this Community are comprised of Indigenous Knowledge emanating from communities in the neighborhoods of Kabale University. These are communities in the great Kigezi Region.
  • This community holds students (Graduates) dissertation and Thesis, Staff field reports, Students (undergraduate) study reports
  • The community includes research article publications in journals both local and international, conference papers in proceedings and reports, abstracts and reviews by Kabale University Staff and Students
  • This community archives publications by individual University Staff and Students, Faculty and Departmental Publications (i.e. University Journal, Newsletters, University official publications etc.), groups and Association operating in the University (i.e. Convocation and Staff and Students Association}

Recent Submissions

ItemRestricted
Impact of food and beverage management on customer satisfaction in the hospitality sector: A case study of White Horse Inn Hotel, Kabale District
(Kabale University, 2024) Tumusiime, Cosmas Bwambale
Researching on customer satisfaction is important because satisfied customers become loyal customers. Therefore, it is crucial to measure customer satisfaction towards food and beverage management because satisfied customers make repetitive purchasing and recommendations to others that will make profits of that particular hospitality establishment. Customer satisfaction with food and beverage management can significantly be influenced by food and beverage presentation, image and physical environment. Hence, earlier, many studies have shown the relationship between food and beverage management and customer satisfaction. But still, limited literature has been focused on the impact of the confirmation of customer expectation on the relationship between food and beverage management and customer satisfaction. Hence, this study aims to measure customer satisfaction based on the food and beverage presentation, image and physical environment. A total of 200 questionnaires were distributed to customers and staff at White Horse Inn Hotel in Kabale district . Totally 133 questionnaires were used for further analysis out of 200, representing a response rate of 66.5%. The result of the study revealed that food and beverage presentation has a significant and positive relationship with confirmation of customers’ expectations and in turn, their satisfaction level towards food and beverage management. Implications and directions for future research are also highlighted in this present study.
ItemOpen Access
Representation of Culture and Human Rights Violations in Timothy Wangusa’s Upon This Mountain and Austin Bukenya’s The Bride. Unisa Press.
(Unisa Press, 2024) Tugume, Benon.
This article examines the portrayal of culture and human rights violations in Timothy Wangusa’s novel, Upon This Mountain and Austin Bukenya’s play, The Bride. It focuses on the Bagisu cultural ritual of circumcision in Upon This Mountain as well as the culture-based traditions of prejudice and discrimination in The Bride that are responsible for the violation of the rights of Kangala, Wabwire, and Mwambu in the former, and Namvua and her entire Merio family in the latter. In this article, I apply qualitative methods of data collection and analysis since it is a case study of Wangusa’s Upon This Mountain and Bukenya’s The Bride as primary texts. Data for analysis is generated by carrying out a close reading of the primary texts as well as secondary texts—critical works, journal articles, and literature on human rights purposely to strengthen the discussion of culture and human rights violations depicted in the primary texts. The reading of primary texts focuses on characters and themes since the objectives are twofold: first, to examine the point of view of individual characters subjected to ritual pain, trauma, and intra-cultural discrimination in Upon This Mountain and second, to analyse the writer’s use of dialogue and action to dramatise resistance to cultural prejudices and discrimination in The Bride. Using principles of human rights, the paper discusses the pain, torture, and degrading treatment Kangala and Wabwire in Upon This Mountain go through as they submit to the ritual of the knife. Similarly, the article explores discrimination against Namvua and her entire Merio family based on age-old cultural prejudices in The Bride. Lekindo, the leader of the young generation is opposed to her discrimination and fights for her rights and acceptance in the plains by smashing the skull, an iconic symbol of cultural beliefs. He marries Namvua to underscore the theme of the inevitability of change because of human rights abuses.
ItemRestricted
Dhima ya Mbinu ya Ucheshi Katika Fasihi: Uchunguzi Kifani Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani.
(Kabale University, 2024) Atwijukire, Beatrice
Utafiti huu ulilenga kuchunguza dhima ya mbinu ya ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha mbinu za ucheshi zinazojitokeza katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani, kueleza ufanano na utofautianaji wa ujitokezaji wa ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani na kutathmini dhima ya ucheshi katika kujenga maudhui katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umtindo iliyoasisiwa na Leech (1969). Nadharia hii hushikilia kwamba kazi za fasihi haziwezi kueleweka bila lugha. Kwa hivyo, jinsi ilivyotumiwa na msanii kuumba kazi yake ni aula msingi kabisa kwa uelekeo wa nadharia hii. Wango la utafiti huu ni Diwani tatu za Euphrase Kezilahabi ambazo ni Kichomi (1974), Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Sababu ya kuteua Diwani hizi ni kuwa Kezilahabi ni mshairi maarufu katika historia na maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. Utafiti ulitumia usampulishaji nasibu tabakishi. Diwani za Kezilahabi zilitabakishwa kulingana na mwaka zilimochapishwa na zile zilizotungwa hivi karibuni ndizo zilizoteuliwa yaani Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Data zilikusanywa na kupangiliwa vizuri kulingana na mada kuu na ndogondogo ambazo zilibuniwa kutoka Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani kwa kuzingatia madhumuni mahususi ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba mbinu za ucheshi kama majina ya majazi, misemo, taswira za kuchekesha, tanakali sauti, uradidi, na utohozi zinajitokeza kwa namna mbalimbali katika Diwani hizi mbili. Kila moja ikichangia kwa namna yake katika kujenga maudhui na kuwasilisha malengo ya mwandishi. Pia ucheshi unathibitisha kuwa ni chombo muhimu katika fasihi, si tu kwa ajili ya burudani bali pia kwa ajili ya kufikisha ujumbe muhimu kwa jamii. Kwa mfano ucheshi huonesha matendo maovu ya viongozi, hali ya maisha ya watu katika jamii nakadhalika. Kwa njia hii, mashairi haya yanajenga maudhui yanayovutia na yenye kuleta mwanga juu ya masuala ya kijamii na kibinadamu kwa namna inayoeleweka na kukubalika na wasomaji. Utafiti ulipendekeza kwamba watafiti watakaofuata wa kazi za fasihi waendelee kuchunguza namna mbinu za ucheshi zinavyoweza kuendelezwa kwa ubunifu ili kuvutia wasomaji na kuwasilisha maudhui yenye thamani kwa jamii.
ItemRestricted
Dosari Za Kifonolojia Zinazojidhirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Katika Jamii Ya Wachiga: Uzingativu Wa Muktadha Wa Kujifunzia.
(Kabale University, 2024) Turigye, Rosemary
Utafiti huu unahusu dosari za kifonolojia zinazojitokeza miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Kichiga. Lengo lilikuwa kutalii ili kuona muktadha wa kijamii unavyoukilia ujitokezaji wa dosari hizo za kifonolojia. Kwa mahsusi kabisa, utafiti huu ulilenga kubainisha dosari za kifonolojia, kuelewa chanzo chake, kuzingatia muktadha wa kujifunza, na kutoa mapendekezo ya mikakati inayoweza kutumika kupunguza dosari hizo. Utafiti ulitumia sampuli ya watoa taarifa 94 waliogawanyika katika sehemu mbili, walimu 10 na wanafunzi 84. Mbinu za kukusanya data zilizotumika ni uandishi wa insha na hojaji. Hojaji zilitumika kwa walimu na wanafunzi wakati uandishi ulitumika kwa wajifunzaji lugha. Utafiti uliongozwa na Nadharia Uchanganuzi Makosa na Nadharia Elekezi hasa kwa mahsusi wake muhimili wa ingizo. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa dosari za udondoshaji, uchopekaji na ubadilishaji wa sauti zilibainika. Utafiti umebaini kuwa chanzo cha dosari hizo ni pamoja na uhamishaji, athari za lugha ya Kichiga, utamaduni wa Kichiga na ukakamaaji. Vilevile, imebainika kwamba, muktadha wa kijamii unachochea kwa kiasi kikubwa uibuzi wa dosari za kifonolojia kutokana na ukosefu wa uibuzi wa ingizo ndani ya mazingira miongoni mwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii. Muktadha wa kujifunzia uligunduliwa kuwa una athari kubwa kwa ujitokezaji wa dosari za kifonolojia, kwani wajifunzaji walikuwa wakipata changamoto kutokana na ukosefu wa mazoezi na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mazingira yao ya kila siku. Aidha, mikakati anuwai ilipendekezwa ili kupunguza dosari za kifonolojia, kuongeza mazoezi ya kusikiliza na kuzungumza Kiswahili, kuboresha vifaa vya kufundishia na kujifunzia, na kuanzisha programu za msaada kwa wajifunzaji wenye dosari za kifonolojia. Kwa kufanya hivyo, inatarajiwa kuwa dosari za kifonolojia zinaweza kupunguzwa na ujuzi wa lugha ya Kiswahili unaweza kuboreshwa miongoni mwa wajifunzaji katika jamii ya Kichiga.
ItemRestricted
Matumizi ya Mbinu ya Utanzia na Uibuaji wa Maudhui Katika Tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani.
(Kabale University, 2024) Mundu, Alamira Priscilla
Tasnifu hii inahusu Matumizi ya mbinu ya utanzia na uibuaji wa maudhui katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya mbinu ya utanzia katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa matatu. Lengo la kwanza lilikuwa ni kuchambua matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia teule. Lengo la pili lilikuwa ni kufananisha na kutofautisha sifa bainifu za kitanzia, na lengo la tatu lilikuwa ni kutathmini maudhui yanayoibuliwa na matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia hizo. Wango la utafiti huu ni jumla ya tamthilia za Pauline Kea na Kithaka wa Mberia ambazo idadi yake ni sita. Tamthilia hizi zimegawika katika makundi mawili. Kundi la kwanza linahusu tamthilia tano za Kithaka wa Mberia ambazo ni: Natala 1997,Mchezo wa Karata, 1997, Bara Jingine, 2001, Kifo Kisimani, 2001 na Maua kwenye Jua la Asubuhi 2004. Miongoni mwa tamthilia hizi tatu mtafiti aliteua tamthilia ya Kifo Kisimani. Kundi la pili ni tamthilia ya Pauline Kea ya ni Kigogo 2016. Sampuli ya utafiti ni tamthilia mbili za Kigogo na Kifo Kisimani. Mchakato uliotumika kupata Sampuli ya utafiti ni usampulishaji lengwa na usampulishaji tabakishi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia kifaacha orodha hakiki, zikachambuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti uliongozwa na nadharia ya uhalisia wa Kijamaa. Matokeo yanabainisha kuwa matukio halisi katika tamthilia teule ni pamoja na; utokeaji wa vifo, kuibuka kwa magonjwa katika jamii, kufungwa kwa wahusika. Hali kadhalika, sifa bainifu za kitanzia ni kama vile; mhusika nguli anayetoka katika tabaka la juu, migogoro, matukio yanayoamsha hisia za woga, huzuni na huruma na Mwisho mbaya wa mhusika nguli. Maudhui yaliyoibulliwa na matukio halisi ya kitanzia ni pamoja na, ukiukwaji wa haki za binadamu, uongozi mbaya, ukatili, umaskini, tamaa na ubinafsi. Tafiti zaidi zinaweza kufanywa kwa kuangalia vipengele vingine au mbinu nyingine. Mbinu zinazoweza kuchambuliwa ni pamoja na ujensi ubabe dume katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani, maudhui makuu katika tamthilia teule na mbinu nyinginezo katika tamthilia hizo. Pia utafiti unaweza kufanyika kwa kutumia nadharia nyingine kama vile nadharia ya ufeministi.