Usawiri Wa Mwanamke Katika Methali Za Kikonzo.
Loading...
Date
2024
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kabale University
Abstract
Utafiti huu ulihusuUsawiri wa mwanamke katika methali za Kikonjo.Utafiti huu ulifanyiwa katika kata la Bwera wilayani Kasese. Kwa kutumia njia ya mahojiano, sampuli ya wazee ishirini (20) wenye umri wa miaka hamsini hadi juu ilitumiwa ili kufikia lengo la kwanza la pili na la tatu. Methali mbali mbali za Kikonjo zilikusanywa na kutengenezewa tafsiri isiyo rasimi katika Kiswahili ili kutimiza lengo la kwanza.Ili kufikia lengo la pili, uchunguzi makinifu ulifanywa na mtafiti akishirikiana na wazee ili kuona jinsi mwanamke anavyosawiriwa katika methali hizo kwa mfano kama asiye na mapenzi ya dhati, chombo cha starehe, mtumwa, mvivu, na mtu asiye na siri na kadhalika. Kwa lengo la tatu, mtafiti alifanya mahojiano kwa wazee ili kupata sababu za mwanamke kusawiriwa anavyosawiriwa katika methali za Kikonjo kwa mfano utamaduni, diini, tabia za mwanamke, na kadhalika.
Description
Keywords
Usawiri, Mwanamke, Katika Methali, Kikonzo
Citation
Ithungu, Roseline (2024). Usawiri Wa Mwanamke Katika Methali Za Kikonzo. Kabale: Kabale University.