Uchunguzi Linganishi wa Usawiri wa Mwanamke Katika Jamii ya Wanyankore na Tamthilia ya Mama Ee Ya Ari Katini Mwachofi.

Loading...
Thumbnail Image

Date

2024

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Kabale University

Abstract

Utafiti huu ulihusu Uchunguzi linganishi wa usawiri wa mwanamke katika jamii ya Wanyankore na katika tamthilia ya Mama ee iliyoandikwa na Ari Katini Mwachofi. Kwa kutumia mbinu ya mahojiano, mtafiti alipata data za lengo la kwanza na la tatu. Kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi nyaraka, mtafiti alipata data za lengo la pili na la tatu. Sampuli ya watu kumi na watano yaani wanawake watano kutoka kila kijiji teule katika kata la Ruhaama ndio walifanya kama watoa taarifa pia data nyingine zikatolewa kwa tamthilia ya Mama ee iliyoandikwa na Ari Katini Mwachofi. Matokeo ni kwamba Jamii ya Wanyakore mwanamke anadunishwa ingawa kwa upande mdogo anakweza, pili yalionyesha kwamba mwanamke katika Tamthilia ya Mama ee anatwezwa kwa upande mkubwa.Mtafiti anapendekeza kwamba tafiti nyingine zifanywe kuhusu suala hili kwa kuangazia tamthilia,riwaya,diwani na tungo nyingine za kifasihi ili kuwepo uelewekaji wake zaidi.

Description

Keywords

Uchunguzi Linganishi, Usawiri, Mwanamke, Jamii, Wanyankore, Tamthilia, Mama, Katini Mwachofi

Citation

Akampamya, Mauricia (2024). Uchunguzi Linganishi wa Usawiri wa Mwanamke Katika Jamii ya Wanyankore na Tamthilia ya Mama Ee Ya Ari Katini Mwachofi. Kabale: Kabale University.