Methali Kama Kielezo Cha Shughuli Katika Jamii Ya Wahororo/ Wakiga Wilayani Rukungiri Nchini Uganda.

Loading...
Thumbnail Image

Date

2021

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Kabale University

Abstract

Utafiti huu unahusu methali kama kielezo cha shughuli katika jamii ya Wahororo/ Wakiga wilayani Rukungiri, nchini Uganda. Hivyo ni kwamba somo hili liliongozwa na lengo kuu ambalo lilikuwa ni kubainisha shughuli zinazoelezwa na methali za kihororo pamoja na zile za Kikiga wilayani Rukungiri.Somo hili pia lilifuata malengo mahususi ambayo yalikuwa ni pamoja na: Kwanza, utafiti huu ulichunguza shughuli zinazoweza kuelezwa na methali katika Wahororo Wakiga nchini Uganda. Pili, utafiti huu ulibainisha uhusiano kati ya methali na matawi mengine ya fasihi simulizi na jinsi yanavyoweza kutumiwa kama kielezo cha shughuli za jamii ya Wahoro/Wakiga, nchini Uganda. Tatu, utafiti huu ulibainisha changamoto zinazokumba methali kama kielezo cha shughuli katika Wahororo/Wakiga wilayani Rukungiri pamoja na njia za kukabiliana na changamoto zinazokumba methali kutumiwa kama vielezo vya shughuli za Wahororo/ Wakiga wilayani Rukungiri. Utafiti huu ulifanyiwa wilayani Rukungiri katika vijiji vya Eisherero, Nyabihinga, Omukarere pamoja na Nyakashaka. Wahojiwa wazazi walitumiwa katika utafiti huu wakati wa kutoa data, walisaidia katika kutoa data kuhusu shughuli zinazoelezwa na methali pamoja na mifano ya methali zinazoeleza shughuli hizo. Utafiti huu uligundua kuwa ingawa methali hukumbwa na changamoto tofauti tofauti, zinarejelewa sana kama kielezo cha shughuli za Wahororo/Wakiga.

Description

Keywords

Methali, Kama Kielezo, Shughuli Katika Jamii, Wahororo, Wakiga Wilayani, Rukungiri, Uganda

Citation

Nahurira, Ronnet (2021). Methali Kama Kielezo Cha Shughuli Katika Jamii Ya Wahororo/ Wakiga Wilayani Rukungiri Nchini Uganda. Kabale: Kabale University.