Nafasi ya Leksikoni yenye Vipashio Ghairi kutoka Kiingereza na Kiarabu katika Fonolojia ya Leksikoni ya Kiswahili Sanifu

Abstract

Makala haya yanahusu ubainishaji wa nafasi ya leksikoni ya mkopo yenye vipashio ghairi katika leksikoni ya Kiswahili sanifu. Data zilizotumiwa katika makala haya zilikusanywa kutoka makavazi ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mbinu za uhakiki matini na usomaji nyaraka zilitumiwa kukusanya data. Uhusiano wa matabaka ya leksikoni ya Kiswahili umeelezwa kwa kutumia modeli ya uhusiano wa KIINI-PEMBEZONI ya Itô na Mester (1995) sambamba na Nadharia ya Umbo Upeo (UU). Data imedhihirisha kuwa leksikoni ya Kiswahili inatoa ushahidi kuwa kuna matabaka mbalimbali ndani yake. Modeli iliyotumiwa imetuwezesha kubainisha mwingiliano taratibu na utabakishi wa leksikoni ya Kiswahili. Leksikoni ya Kiswahili yenye viambajengo ghairi husika imetambuliwa kisinkronia kwa kuwa viambajengo hivyo vina mchango katika sarufi ya Kiswahili (fonolojia ya leksikoni ya Kiswahili) hasa kuhusiana na mashartizuizi ya kimuundo. Matokeo yamebainisha kuwa mashartizuizi ya leksikoni ya Kiswahili iliyopokelewa kutoka Kiingereza na Kiarabu na viambajengo ghairi yanafanya kazi katika mawanda ya PEMBEZONI.

Description

Keywords

Citation