Nafasi ya Leksikoni yenye Vipashio Ghairi kutoka Kiingereza na Kiarabu katika Fonolojia ya Leksikoni ya Kiswahili Sanifu

dc.contributor.authorDavid, Majariwa
dc.date.accessioned2023-04-20T13:06:30Z
dc.date.available2023-04-20T13:06:30Z
dc.date.issued2023-03
dc.description.abstractMakala haya yanahusu ubainishaji wa nafasi ya leksikoni ya mkopo yenye vipashio ghairi katika leksikoni ya Kiswahili sanifu. Data zilizotumiwa katika makala haya zilikusanywa kutoka makavazi ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mbinu za uhakiki matini na usomaji nyaraka zilitumiwa kukusanya data. Uhusiano wa matabaka ya leksikoni ya Kiswahili umeelezwa kwa kutumia modeli ya uhusiano wa KIINI-PEMBEZONI ya Itô na Mester (1995) sambamba na Nadharia ya Umbo Upeo (UU). Data imedhihirisha kuwa leksikoni ya Kiswahili inatoa ushahidi kuwa kuna matabaka mbalimbali ndani yake. Modeli iliyotumiwa imetuwezesha kubainisha mwingiliano taratibu na utabakishi wa leksikoni ya Kiswahili. Leksikoni ya Kiswahili yenye viambajengo ghairi husika imetambuliwa kisinkronia kwa kuwa viambajengo hivyo vina mchango katika sarufi ya Kiswahili (fonolojia ya leksikoni ya Kiswahili) hasa kuhusiana na mashartizuizi ya kimuundo. Matokeo yamebainisha kuwa mashartizuizi ya leksikoni ya Kiswahili iliyopokelewa kutoka Kiingereza na Kiarabu na viambajengo ghairi yanafanya kazi katika mawanda ya PEMBEZONI.
dc.description.sponsorshipKabale University
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/1138
dc.language.isoen
dc.titleNafasi ya Leksikoni yenye Vipashio Ghairi kutoka Kiingereza na Kiarabu katika Fonolojia ya Leksikoni ya Kiswahili Sanifu
dc.typeArticle

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Nafasi ya Leksikoni yenye Vipashio Ghairi katika Fonolojia ya Leksikoni ya Kiswahili Sanifu.pdf
Size:
446.11 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: