Kabale University Digital Repository (KAB-DR)
    • Login
    View Item 
    •   KAB-DR Home
    • Research Articles
    • Institute of Languages (INSTL)
    • View Item
    •   KAB-DR Home
    • Research Articles
    • Institute of Languages (INSTL)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Upokeaji na Ukubalifu wa Vitamkwa vya Kiarabu na Kiingereza katika Fonolojia ya Kiswahili

    Thumbnail
    View/Open
    Main Articles (1.130Mb)
    Date
    2021
    Author
    David, Majariwa
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Makala hii inachunguza jinsi vitamkwa vya kigeni [χ], [ɣ], [ð] na [θ] vilivyopokelewa katika fonolojia ya Kiswahili kutoka Kiarabu na Kiingereza. Lengo la makala hii ni kuelezea sababu za ukubalifu2 wa vitamkwa hivyo katika mfumo wa fonolojia ya Kiswahili, licha ya mifumo ya fonolojia ya lugha kufikiriwa kuwa thabiti zaidi dhidi ya mabadiliko. Data zilizotumika zilipatikana kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) (2013) Toleo la Tatu na Bosha (1993). Nadharia ya Umbo Upeo imetumika katika uchanganuzi wa data za makala hii. Kuna mikakati ya urekebishaji kadhaa ambayo inaelezea jinsi vitamkwa vinavyoshughulikiwa katika upokeaji wa maneno ya mkopo katika muktadha wa nadharia hii. Hata hivyo, ilibainika kuwa vitamkwa vya kigeni [χ], [ɣ], [ð] na [θ] vilighairi mikakati hiyo ya urekebishaji na kupenyeza katika fonolojia ya Kiswahili. Upokeaji wa vitamkwa hivyo uliwezekana kupitia upangiliaji upya wa mashartizuizi ya Kiswahili katika Umbo Upeo. Vitamkwa vilivyopokelewa vilikubalika katika mfumo wa orodha ya konsonanti za Kiswahili kwa kuzingatia msingi wa iktisadi ya sifa na mvutano pande mbili. Vitamkwa hivyo vilipokelewa kutokana na kuwapo kwa mapengo ya vitamkwa hivyo katika orodha ya vitamkwa vya Kiswahili.
    URI
    http://hdl.handle.net/20.500.12493/617
    Collections
    • Institute of Languages (INSTL) [9]

    KAB-DR
    Contact Us | Send Feedback
    Kabale University
     

     

    Browse

    All of KAB-DRCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    KAB-DR
    Contact Us | Send Feedback
    Kabale University