Upokeaji na Ukubalifu wa Vitamkwa vya Kiarabu na Kiingereza katika Fonolojia ya Kiswahili

dc.contributor.authorDavid, Majariwa
dc.date.accessioned2022-04-11T06:11:57Z
dc.date.available2022-04-11T06:11:57Z
dc.date.issued2021
dc.description.abstractMakala hii inachunguza jinsi vitamkwa vya kigeni [χ], [ɣ], [ð] na [θ] vilivyopokelewa katika fonolojia ya Kiswahili kutoka Kiarabu na Kiingereza. Lengo la makala hii ni kuelezea sababu za ukubalifu2 wa vitamkwa hivyo katika mfumo wa fonolojia ya Kiswahili, licha ya mifumo ya fonolojia ya lugha kufikiriwa kuwa thabiti zaidi dhidi ya mabadiliko. Data zilizotumika zilipatikana kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) (2013) Toleo la Tatu na Bosha (1993). Nadharia ya Umbo Upeo imetumika katika uchanganuzi wa data za makala hii. Kuna mikakati ya urekebishaji kadhaa ambayo inaelezea jinsi vitamkwa vinavyoshughulikiwa katika upokeaji wa maneno ya mkopo katika muktadha wa nadharia hii. Hata hivyo, ilibainika kuwa vitamkwa vya kigeni [χ], [ɣ], [ð] na [θ] vilighairi mikakati hiyo ya urekebishaji na kupenyeza katika fonolojia ya Kiswahili. Upokeaji wa vitamkwa hivyo uliwezekana kupitia upangiliaji upya wa mashartizuizi ya Kiswahili katika Umbo Upeo. Vitamkwa vilivyopokelewa vilikubalika katika mfumo wa orodha ya konsonanti za Kiswahili kwa kuzingatia msingi wa iktisadi ya sifa na mvutano pande mbili. Vitamkwa hivyo vilipokelewa kutokana na kuwapo kwa mapengo ya vitamkwa hivyo katika orodha ya vitamkwa vya Kiswahili.en_US
dc.description.sponsorshipKabale Universityen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/617
dc.publisherJarida la Taasisi ya Taaluma za Kiswahilien_US
dc.subjectUpokeaji na Ukubalifu wa Vitamkwa vya Kiarabu na Kiingerezaen_US
dc.titleUpokeaji na Ukubalifu wa Vitamkwa vya Kiarabu na Kiingereza katika Fonolojia ya Kiswahilien_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Upokeaji na Ukubalifu wa Vitamkwa vya Kiarabu na Kiingereza katika Fonolojia ya Kiswahili.pdf
Size:
1.13 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Main Articles
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: