Institute of Languages (INSTL)
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Institute of Languages (INSTL) by Author "Amanzi, Musa .O."
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Open Access Miktadha ya Kisintaksia itokanayo na Makusudio ya Mawasiliano katika Uibuzi wa Miundo Virai Kubalifu ya Kiswahili.(Kabale University, 2024) Amanzi, Musa .O.Lugha ya Kiswahili ni lugha yenye muundo wa kitenzi kati yaani, katika sentensi ni lazima kuwe na viambajengo kabla au baada ya kitenzi ambavyo vinaweza kuwa dhahiri au visiwe dhahiri. Kuwapo kwa muundo huu hakumaanishi kuwa lugha hii ina utaratibu mmoja kiusemaji. Bali, ipo miundo mingine ambayo kimsingi ujitokezaji wake husababishwa na miktadha mbalimbali ya kisintaksia. Makala haya kwahiyo yanalenga kuchunguza miktadha ya kisintaksia itokanayo na makusudio ya mawasiliano katika uibuzi wa miundo virai kubalifu vya sentensi za Kiswahili. Data za makala haya zilipatikana uwandani kupitia mbinu ya ushuhudiaji sikizi na mahojiano. Nadharia ya Uchunguzi wa Kimaeneo ya Joshua Aaron Fishman mwaka (1972) ilitumika katika uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Katika uwasilishaji wa kila data, alama “Mt.” ilitumika ikimaanisha “mtoataarifa”. Matokeo ya makala haya yanaonesha kuwa kuna miktadha sita ya kisintaksia itokanayo na makusudio ya mawasiliano katika uibuzi wa miundo virai kubali vya sentensi za Kiswahili. Miktadha hiyo ni umadaishaji, ufokasilishaji, usititizi, uulizi, maombi na kuagiza. Aidha, makala haya yanapendekeza kuwa tafiti nyingine zifanyike ili kuchunguza miundo virai kubalifu itokanayo na miktadha ya kisintaksia ya makusudio ya mawasiliano.