Dhima ya Methali Ktika Ukuzaji wa Nidhamu Baina ya Wanajamii Kijijini Bungandaro, Wila Yani Rubanda Nchini Uganda.
Loading...
Date
2022
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kabale University
Abstract
Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza dhirna ya methali katika ukuzaji wa nidhamu baina ya wanajamii kijijini Bungandaro, wilayani Rubanda nchini Uganda. Dhima za methali katika ukuzaji wa nidhamu zilichunguzwa katika utafiti huu. Aidha utafiti huu umeziainisha methali katika makundi matatu makuu, yaani uainishaji huu hutegemea rnaana ya ndani pamoja na maana ya nje na walengwa wa rnethali husika. Vile vile, methali zirneainishwa kulingana na maudhui ya kimsingi yanayowasilishwa ndani ya methali hiyo hiyo, pamoja na uainisho wa kimafunzo. Makundi hayo ni pamoja na: Methali za kukashifu tabia mbaya miongoni mwa wanajamii, Methali za kuhimiza heshima kwa wazima miongoni mwa wanajamii pamoja na Methali za kuleta amani miongoni mwa wanajamii. Basi, makundi haya yote hukuza na kutimiza swala la nidhamu baina ya wanajamii. Utafiti huu umeundwa na sura tano yaani sura ya kwanza, pili, tatu, nne na tano. Sura ya Kwanza imeshughulikia Utangulizi, Tatizo la utafiti, Malengo ya Utafiti, Upeo wa utafiti, Umuhimu wa Utafiti na Changamoto zilizoukabili utafiti huu. Sura ya Pili imeshughulikia Mapitio ya Kitaaluma na ya Kazi tangulizi ambapo imeelezea yaliyoandikwa kuhusu methali na jinsi zinavyoweza kukuza nidhamu baina ya wanajamii. Aidha, imeelezea yaliyoandikwa kuhusu makundi pamoja na uanisho wa methali katika hali au masuala tofauti tofauti. Kadhalika, sura ya pili irneelezea Pengo la Maarifa na Kiunzi cha utafiti wa awali pamoja na jinsi utafiti huu ulivyoziba kiunzi au pengo li'ilo. Sura ya Tatu irnezungumzia Njia na Mbinu za Uafiti. Imezungumzia Utangulizi, Eneo la Utafiti, Sampuli ya Utafiti na Usampulishaji, Ukusanyaji wa Data. Uchambuzi wa Data na Vifaa vya Utafiti.Sura ya Nne imeeleza juu ya Uwasilishaji na Uchambuzi wa data,ambapo imeelezea aina za teknolojia ambazo huwa na dhima katika ukuzaji wa nidhamu. Sura ya tano imeeleza juu ya Muhtasari wa Utafiti na Mapendekezo.
Description
Keywords
Dhima, Methali, Ktika, Ukuzaji, Nidhamu, Baina, Wanajamii, Kijijini, Bungandaro, Rubanda Nchini, Uganda
Citation
Atwiniramasiko, Ivan (2022). Dhima ya Methali Ktika Ukuzaji wa Nidhamu Baina ya Wanajamii Kijijini Bungandaro, Wila Yani Rubanda Nchini Uganda. Kabale: Kabale University.