Uchanganuzi Wa Utabaka Katika Tamthilia Ya Kilio Cha Haki Ya Alamin Mazrul.

Loading...
Thumbnail Image

Date

2023

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Kabale University

Abstract

Utafiti huu ulichunguza kuhusu "Uchanganuzi wa Utabaka Katika Tamthilia ya Kilio Cha Haki ya (Alamin Mazrui) ". Suala la utafiti huu lilikuwa: Watu katika jamii nyingi hasa hasa za kiafrika huathirika sana na athari za matabaka. Kwa sababu katikajamii nyingi kuna makabaila, kuna wale ambao waweza afadhali kukidhi mahitaji yao na kuna wale ambao hawajiwezi kabisa . Unapochunguza katika tamthilia ya Kilio cha Haki ya Ali Mazrui kuna makundi ya watu mbalimbali kama vile; wanacho, wanaojikidhi kimaisha na wasiojiweza . Suala la utabaka ni suala nyeti katika fasihi ya Kiswahili. Suala hili la utabaka limejitokeza mno katika uandishi wa Ali Mazrui ingawa hakuna watafiti ambao warneishalichunguza. Hii ndiyo sababu utafiti huu ulikusudia kutarnbulisha uhusiano uliopo baina ya matabaka rnbalimbali yanayojitokeza katika tamthilia ya Kilio cha Haki, kubainisha rnchango wa migogoro kati ya matabaka yaliyomo pamoja na kutathmini masuala yanayopigiwa vita na migogoro kati ya matabaka mbalimbali yaliyomo katika tamthilia hii kama vinavyoelezewa na mtunzi. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usornaji makini na uchunguzaji wa tamthilia ya Kilio cha Haki kwa kuisoma na kuichambua kwa kina na kuiwasilisha data kwa mbinu ya kiuthamano. Katika utafiti huu, mtafiti amegundua kwamba nchini Kenya kulingana na tamthilia ya Kilio cha Haki, kuna matabaka makuu rnawili ya walionacho na wasionacho. Tabaka la walionacho hujumuisha wahusika kama; Delamon, Tereki, Shindo, Matovu, Zari na Kimbo na tabaka la wasionacho hujumuisha wahusika kama; Lanina, Dewe, Musa na wengine. Hawa wanaendelea kutambika kwa kuongozwa vibaya, kulipwa mshahara duni, kunyanyaswa, kutonzwa kitu kidogo iii wasaidiwe, kulaumiwa na kutamauka. Mtafiti pia amegundua baadhi ya mambo rnbalirnbali yanayopigiwa vita na mwandishi katika tamthilia ya Kilio cha Haki pamoja na jam ii mbalimbali za kiafrika. Jarnbo la kwanza linalopigiwa vita ni rushwa pamoja na athari zake kwani rushwa irnesababisha vijitabia vingi vikiwerno, uchafu wa mazingira, dharau, uvundo nidharnu, pamoja na malalamiko ya kutamauka. Vile, suala jingine linalopigiwa vita na rnwandishi Alamin Mazrui ni utabaka. Utafiti huu una umuhimu rnkubwa katika uwanja wa fasihi. Hii ni kwa sababu ulikuwa ni wa kwanza kuchunguza utabaka katika tamthilia ya Kilio cha Haki ya (Alamin Mazrui), Zaidi ya hayo, utafiti huu utakuwa dira na mwongozo kwa watafiti wengine watakaochunguza zaidi kuhusu utabaka.

Description

Keywords

Uchanganuzi, Utabaka, Tamthilia, Kilio Cha Haki, Alamin Mazrul

Citation

Tayebwa, Novias (2023). Uchanganuzi Wa Utabaka Katika Tamthilia Ya Kilio Cha Haki Ya Alamin Mazrul. Kabale: Kabale University.