Uchunguzi wa Changamoto za Kufundisha Fasihi ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Kiwango cha Chini Katika Shule za Upili Zilizochaguliwa Wilayani Kabale.

dc.contributor.authorNabasa, Mackline
dc.date.accessioned2025-01-17T09:30:31Z
dc.date.available2025-01-17T09:30:31Z
dc.date.issued2024
dc.description.abstractUtafiti huu umefanywa Wilayani Kabale. Madhumuni ya utafiti yalikuwa; kuchunguza changamoto za kufundisha fasihi ya Kiswahili Kwa wanafunzi wa kiwango cha chini katika shule zilizochaguliwa wilayani Kabale. Muundo wa uchunguzi na maelezo ulitumiwa. Walengwa walikuwa wanafunzi, walimu wa Kiswahili na walimu wakuu kutoka shule ya upili ya Trinity, shule ya sekondari ya Kabale, shule ya Rock, shule ya Brainstorm. Mbinu ya usampulishaji nasibu ilitumika katika kuchagua sampuli ya idadi ya watu. Mbinu za kukusanya data zilikuwa mahojiano kwa wanafunzi, hojaji kwa walimu wa Kiswahili na walimu wakuu. Data zilikusanywa kutoka shuleni kwa kutumia dodoso iliyoundwa. Kisha data ilichakatwa katika idadi ya wahojiwa, asilimia katika jedwali na maelezo. Matokeo yalikusudiwa kuwaongoza wadau katika kutafuta njia za kuepuka changamoto za kufundisha fasihi ya Kiswahili kwa wanafunzi wa kiwango cha chini. Kutokana na matokeo ya utafiti, mazingira ya kujifunzia na upatikanaji wa nyenzo za kujifunzia huathiri ufundishaji wa fasihi ya Kiswahili. Hata hivyo, utafiti uligundua kuwa mazingira ya kujifunzia bila nyenzo za kujifunzia huathiri ufundishaji wa fasihi ya Kiswahili. Kutokana na hali hiyo, utafiti ulisisitiza kuwa ili kuboresha ufundishaji wa fasihi, vifaa vya kijifunzia viwekewe katika mazingira ya kufundishia, kuanzisha maktaba yenye vifaa vya kutosha. Utafiti unapendekeza mikakati ya kuepuka changamoto za kufundisha fasihi ya Kiswahili kwa wanafunzi wa kiwango cha chini. Sekta ya elimu inapaswa kufadhiliwa ipasavyo ili kuwezesha sekta hiyo kupata vifaa vinavyohitajika ili kufanya ujifunzaji wa fasihi ya Kiswahili uweze kukidhi kiwango cha juu.
dc.identifier.citationNabasa, Mackline (2024). Uchunguzi wa Changamoto za Kufundisha Fasihi ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Kiwango cha Chini Katika Shule za Upili Zilizochaguliwa Wilayani Kabale. Kabale: Kabale University.
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/2824
dc.language.isoen
dc.publisherKabale University
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United Statesen
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/
dc.subjectUchunguzi
dc.subjectChangamoto
dc.subjectKufundisha Fasihi
dc.subjectKiswahili
dc.subjectWanafunzi
dc.subjectKiwango
dc.subjectChini
dc.subjectShule
dc.subjectUpili Zilizochaguliwa
dc.subjectWilayani Kabale
dc.titleUchunguzi wa Changamoto za Kufundisha Fasihi ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Kiwango cha Chini Katika Shule za Upili Zilizochaguliwa Wilayani Kabale.
dc.typeThesis

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Nabasa Mackline-2024-KED-Research Dissertation.pdf
Size:
702.69 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: