Dhia Ya Methali Katika Ukuzaji Wa Nidhamu Baina Ya W Anajamii Kijijini Bungandaro, Wila Y Ani Rubanda Nchini Uganda
Loading...
Date
2021
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kabale University
Abstract
Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza dhima ya methali katika ukuzaji wa nidhamu baina ya wanajamii
kijijini Bungandaro, wilayani Rubanda nchini Uganda. Dhima za methali katika ukuzaji wa nidhamu
zilichunguzwa katika utafiti huu. Aidha utafiti huu umeziainisha methali katika makundi matatu mak uu, yaani
uainishaji huu hutegemea maana ya ndani pamoja na maana ya nje na walengwa wa methali husika. Vile vile,
methali zimeainishwa kulingana na maudhui ya kirnsingi yanayowasilishwa ndani ya methali hiyo hiyo, pamoja
na uainisho wa kimafunzo. Makundi hayo ni pamoja na: Methali za kukashifu tabia mbaya miongoni mwa
wanajamii, Methali za kuhimiza heshima kwa wazima miongoni mwa wanajamii pamoja na Methali za kuleta
amani miongoni rnwa wanajamii. Basi, makundi haya yote hukuza na kutimiza swala la nidhamu baina ya
wanajamii. Utafiti huu umeundwa na sura tano yaani sura ya kwanza, pili, tatu, nne na tano. Sura ya Kwanza
imeshughulikia Utangulizi, Tatizo la utafiti, Malengo ya Utafiti, Upeo wa utafiti, Umuhimu wa Utafiti na
Changamoto zilizoukabili utafiti huu. Sura ya Pili imeshughulikia Mapitio ya Kitaaluma na ya Kazi tangulizi
ambapo imeelezea yaliyoandikwa kuhusu methali na jinsi zinavyoweza kukuza nidhamu baina ya wanajamii.
Aidha, imeelezea yaliyoandikwa kuhusu makundi pamoja na uanisho wa methali katika hali au masuala tofauti
tofauti. Kadhalika, sura ya pili imeelezea Pengo la Maarifa na Kiunzi cha utafiti wa awali pamoja na jinsi utafiti
huu ulivyoziba kiunzi au pengo hilo. Sura ya Tatu imezungumzia Njia na Mbinu za Utafiti. Imezungumzia
Utangulizi, Eneo la Utafiti, Sampuli ya Utafiti na Usampulishaji, Ukusanyaji wa Data, Uchambuzi wa Data na
Yifaa vya Utafiti.Sura ya Nne imeeleza juu ya Uwasilishaji na Uchambuzi wa data,ambapo imeelezea aina za
teknolojia ambazo huwa na dhima katika ukuzaji wa nidhamu. Sura ya tano imeeleza juu ya Muhtasari wa Utafiti
na Mapendekezo.
Description
Tasnifu Ya Utafiti Iliyotole Wa Kw A Len Go La Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Kuhitimu Shahada Ya Ualjmu Ka Tika
Chuo Kikuu Chakabale.
Keywords
Dhia Ya Methali Katika Ukuzaji Wa Nidhamu Baina Ya W Anajamii Kijijini Bungandaro, Wila Y Ani Rubanda Nchini