Miktadha ya Kisintaksia itokanayo na Makusudio ya Mawasiliano katika Uibuzi wa Miundo Virai Kubalifu ya Kiswahili.

dc.contributor.authorAmanzi, Musa .O.
dc.date.accessioned2024-11-13T07:20:26Z
dc.date.available2024-11-13T07:20:26Z
dc.date.issued2024
dc.description.abstractLugha ya Kiswahili ni lugha yenye muundo wa kitenzi kati yaani, katika sentensi ni lazima kuwe na viambajengo kabla au baada ya kitenzi ambavyo vinaweza kuwa dhahiri au visiwe dhahiri. Kuwapo kwa muundo huu hakumaanishi kuwa lugha hii ina utaratibu mmoja kiusemaji. Bali, ipo miundo mingine ambayo kimsingi ujitokezaji wake husababishwa na miktadha mbalimbali ya kisintaksia. Makala haya kwahiyo yanalenga kuchunguza miktadha ya kisintaksia itokanayo na makusudio ya mawasiliano katika uibuzi wa miundo virai kubalifu vya sentensi za Kiswahili. Data za makala haya zilipatikana uwandani kupitia mbinu ya ushuhudiaji sikizi na mahojiano. Nadharia ya Uchunguzi wa Kimaeneo ya Joshua Aaron Fishman mwaka (1972) ilitumika katika uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Katika uwasilishaji wa kila data, alama “Mt.” ilitumika ikimaanisha “mtoataarifa”. Matokeo ya makala haya yanaonesha kuwa kuna miktadha sita ya kisintaksia itokanayo na makusudio ya mawasiliano katika uibuzi wa miundo virai kubali vya sentensi za Kiswahili. Miktadha hiyo ni umadaishaji, ufokasilishaji, usititizi, uulizi, maombi na kuagiza. Aidha, makala haya yanapendekeza kuwa tafiti nyingine zifanyike ili kuchunguza miundo virai kubalifu itokanayo na miktadha ya kisintaksia ya makusudio ya mawasiliano.
dc.identifier.citationAmanzi, Musa .O. (2024). Miktadha ya Kisintaksia itokanayo na Makusudio ya Mawasiliano katika Uibuzi wa Miundo Virai Kubalifu ya Kiswahili. Kabale: Kabale University.
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/2393
dc.language.isoen
dc.publisherKabale University
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United Statesen
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/
dc.subjectMiktadha ya Kisintaksia
dc.subjectMakusudio ya Mawasiliano
dc.subjectUibuzi wa Miundo Virai Kubalifu
dc.titleMiktadha ya Kisintaksia itokanayo na Makusudio ya Mawasiliano katika Uibuzi wa Miundo Virai Kubalifu ya Kiswahili.
dc.typeArticle

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Amanzi Musa .O.-2024-Research Artilce.pdf
Size:
551.29 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: