Uamilifu wa Sifa katika Mfumo wa Fonimu Konsonanti za Kiswahili.

dc.contributor.authorMajariwa, David
dc.date.accessioned2024-11-13T07:05:54Z
dc.date.available2024-11-13T07:05:54Z
dc.date.issued2024
dc.description.abstractMakala haya yanachunguza uamilifu wa sifa bainifu katika mfumo wa fonimu konsonanti za Kiswahili. Uhakiki wa mfumo wa fonimu konsonanti za Kiswahili ili kubainisha uamilifu wa sifa katika orodha ya fonimu za Kiswahili umeelezwa kwa kuzingatia michakato ya upokeaji wa maneno yenye asili ya Kiarabu mkiwamo vitamkwa [θ], [ð], [χ] na [ɣ]. Uchunguzi huu ulijikita katika misingi ya uhakiki wa orodha ya vitamkwa ambayo ni Udhibiti wa sifa, Iktisadi ya sifa, Uziada, Utabakishi wa sifa na Uzidishaji wa sifa iliyotolewa na Clements (2003). Data zilikusanywa kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la 3 na Bosha (1993). Data zilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi matini. Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kuwa kuna misingi inayodhibiti sifa bainifu za fonimu konsonati za Kiswahili. Kwa ujumla, misingi hii inashirikiana kuukilia kaida za mfumo wa fonimu za Kiswahili kama uelekeo wa msambao wa fonimu na nafasi za kutamkia. Aidha, matokeo yanaonesha kuwa fonimu za Kiswahili zinadhihirisha ruwaza wiani katika mfumo huo. Makala haya yanatoa mchango kwa kubainisha iktisadi kwenye uamilifu wa sifa katika mfumo wa fonimu konsonanti za Kiswahili.
dc.identifier.citationMajariwa, David (2024). Uamilifu wa Sifa katika Mfumo wa Fonimu Konsonanti za Kiswahili. Kabale: Kabale University.
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/2391
dc.language.isoen
dc.publisherKabale University
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United Statesen
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/
dc.subjectUamilifu
dc.subjectSifa
dc.subjectMfumo wa fonimu
dc.titleUamilifu wa Sifa katika Mfumo wa Fonimu Konsonanti za Kiswahili.
dc.typeArticle

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Majariwa David-2024-Research Article.pdf
Size:
657.98 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: