Upenyezaji na Ukubalifu wa Mkururo wa Konsonanti katika Fonolojia ya Kiswahili: Mifano katika Maneno Yaliyopokelewa kutoka Kiingereza na Kiarabu

dc.contributor.authorDavid, Majariwa
dc.date.accessioned2022-05-10T08:39:50Z
dc.date.available2022-05-10T08:39:50Z
dc.date.issued2021
dc.description.abstractMakala haya yanachunguza jinsi mikururo ya konsonanti [Skr-]/[Sk-], [Spr-]/[Sp-], na [Str-]/[St-] ilivyopokelewa katika fonolojia ya Kiswahili kutoka Kiarabu na Kiingereza. Lengo kuu ni kuelezea jinsi mikururo hiyo ya konsonanti ilivyopenyeza na kukubalika katika mfumo wa fonolojia ya Kiswahili. Mifumo ya fonolojia ya lugha inafikiriwa kuwa thabiti zaidi dhidi ya mabadiliko ikilinganishwa na nyanja nyingine za isimu. Data zilizotumika zilipatikana kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) (2013), Toleo la Tatu pamoja na Bosha (1993). Mbinu ya orodhahakiki na usomaji nyaraka zilitumiwa kupata data. Nadharia ya Umbo Upeo ilitumiwa katika uchanganuzi wa data. Uchopezi wa irabu ni mkakati unaozingatiwa sana wakati wa urekebishaji wa mkururo wa konsonanti katika maneno yanayopokelewa katika Kiswahili (Mwita, 2014; Akidah, 2013). Hata hivyo, imebainika kuwa mikururo wa konsonanti [Skr-]/[Sk-], [Spr-]/[Sp-], na [Str-]/[St-] ilighairi mikakati ya urekebishaji na kupenyeza katika fonolojia ya Kiswahili. Upokeaji wa mikururo hiyo ya konsonanti uliwezekana kupitia upangiliaji upya wa mashartizuizi ya Kiswahili. Upangiliaji wa mashartizuizi ulichochewa na haja ya kuwa na uwekevu wa nguvu katika utamkaji. Hivyo, ukubalifu wa mikururo ya konsonanti umeelezwa kupita wepesi wa utamkaji uliochochea upangiliaji wa mashartizuizi ya mfuatano wa konsonanti katika Kiswahili.en_US
dc.description.sponsorshipKabale Universityen_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/618
dc.publisherTaasisi ya Taaluma za Kiswahilien_US
dc.subjectUpenyezaji na Ukubalifu wa Mkururo wa Konsonanti katika Fonolojia ya Kiswahilien_US
dc.titleUpenyezaji na Ukubalifu wa Mkururo wa Konsonanti katika Fonolojia ya Kiswahili: Mifano katika Maneno Yaliyopokelewa kutoka Kiingereza na Kiarabuen_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Upenyezaji na Ukubalifu wa Mkururo wa Konsonanti katika Fonolojia ya Kiswahili..pdf
Size:
674.49 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Main Article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: