Institute of Languages (INSTL)
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Institute of Languages (INSTL) by Title
Now showing 1 - 7 of 7
Results Per Page
Sort Options
Item Restricted Dhima ya Mbinu ya Ucheshi Katika Fasihi: Uchunguzi Kifani Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani.(Kabale University, 2024) Atwijukire, BeatriceUtafiti huu ulilenga kuchunguza dhima ya mbinu ya ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha mbinu za ucheshi zinazojitokeza katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani, kueleza ufanano na utofautianaji wa ujitokezaji wa ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani na kutathmini dhima ya ucheshi katika kujenga maudhui katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umtindo iliyoasisiwa na Leech (1969). Nadharia hii hushikilia kwamba kazi za fasihi haziwezi kueleweka bila lugha. Kwa hivyo, jinsi ilivyotumiwa na msanii kuumba kazi yake ni aula msingi kabisa kwa uelekeo wa nadharia hii. Wango la utafiti huu ni Diwani tatu za Euphrase Kezilahabi ambazo ni Kichomi (1974), Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Sababu ya kuteua Diwani hizi ni kuwa Kezilahabi ni mshairi maarufu katika historia na maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. Utafiti ulitumia usampulishaji nasibu tabakishi. Diwani za Kezilahabi zilitabakishwa kulingana na mwaka zilimochapishwa na zile zilizotungwa hivi karibuni ndizo zilizoteuliwa yaani Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Data zilikusanywa na kupangiliwa vizuri kulingana na mada kuu na ndogondogo ambazo zilibuniwa kutoka Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani kwa kuzingatia madhumuni mahususi ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba mbinu za ucheshi kama majina ya majazi, misemo, taswira za kuchekesha, tanakali sauti, uradidi, na utohozi zinajitokeza kwa namna mbalimbali katika Diwani hizi mbili. Kila moja ikichangia kwa namna yake katika kujenga maudhui na kuwasilisha malengo ya mwandishi. Pia ucheshi unathibitisha kuwa ni chombo muhimu katika fasihi, si tu kwa ajili ya burudani bali pia kwa ajili ya kufikisha ujumbe muhimu kwa jamii. Kwa mfano ucheshi huonesha matendo maovu ya viongozi, hali ya maisha ya watu katika jamii nakadhalika. Kwa njia hii, mashairi haya yanajenga maudhui yanayovutia na yenye kuleta mwanga juu ya masuala ya kijamii na kibinadamu kwa namna inayoeleweka na kukubalika na wasomaji. Utafiti ulipendekeza kwamba watafiti watakaofuata wa kazi za fasihi waendelee kuchunguza namna mbinu za ucheshi zinavyoweza kuendelezwa kwa ubunifu ili kuvutia wasomaji na kuwasilisha maudhui yenye thamani kwa jamii.Item Restricted Dosari Za Kifonolojia Zinazojidhirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Katika Jamii Ya Wachiga: Uzingativu Wa Muktadha Wa Kujifunzia.(Kabale University, 2024) Turigye, RosemaryUtafiti huu unahusu dosari za kifonolojia zinazojitokeza miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Kichiga. Lengo lilikuwa kutalii ili kuona muktadha wa kijamii unavyoukilia ujitokezaji wa dosari hizo za kifonolojia. Kwa mahsusi kabisa, utafiti huu ulilenga kubainisha dosari za kifonolojia, kuelewa chanzo chake, kuzingatia muktadha wa kujifunza, na kutoa mapendekezo ya mikakati inayoweza kutumika kupunguza dosari hizo. Utafiti ulitumia sampuli ya watoa taarifa 94 waliogawanyika katika sehemu mbili, walimu 10 na wanafunzi 84. Mbinu za kukusanya data zilizotumika ni uandishi wa insha na hojaji. Hojaji zilitumika kwa walimu na wanafunzi wakati uandishi ulitumika kwa wajifunzaji lugha. Utafiti uliongozwa na Nadharia Uchanganuzi Makosa na Nadharia Elekezi hasa kwa mahsusi wake muhimili wa ingizo. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa dosari za udondoshaji, uchopekaji na ubadilishaji wa sauti zilibainika. Utafiti umebaini kuwa chanzo cha dosari hizo ni pamoja na uhamishaji, athari za lugha ya Kichiga, utamaduni wa Kichiga na ukakamaaji. Vilevile, imebainika kwamba, muktadha wa kijamii unachochea kwa kiasi kikubwa uibuzi wa dosari za kifonolojia kutokana na ukosefu wa uibuzi wa ingizo ndani ya mazingira miongoni mwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii. Muktadha wa kujifunzia uligunduliwa kuwa una athari kubwa kwa ujitokezaji wa dosari za kifonolojia, kwani wajifunzaji walikuwa wakipata changamoto kutokana na ukosefu wa mazoezi na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mazingira yao ya kila siku. Aidha, mikakati anuwai ilipendekezwa ili kupunguza dosari za kifonolojia, kuongeza mazoezi ya kusikiliza na kuzungumza Kiswahili, kuboresha vifaa vya kufundishia na kujifunzia, na kuanzisha programu za msaada kwa wajifunzaji wenye dosari za kifonolojia. Kwa kufanya hivyo, inatarajiwa kuwa dosari za kifonolojia zinaweza kupunguzwa na ujuzi wa lugha ya Kiswahili unaweza kuboreshwa miongoni mwa wajifunzaji katika jamii ya Kichiga.Item Open Access Education, Enseignement, Pédagogie, Didactique(Revue Della/Afrique, 2023-11-14) Koffi, AGBEFLE G,1- Nature, champs disciplinaires et périodicité de la Revue La revue DELLA se veut une revue scientifique pluridisciplinaire, mieux transdisciplinaire dont les principaux domaines d’intervention sont les lettres, langues, sciences humaines et sociales. En d’autres termes, cette revue est ouverte à la communauté des enseignants et/ou chercheurs en éducation, en linguistique et en didactique des langues qui sont en relation avec un large spectre de sensibilités scientifiques : histoire, sociologie, psychologie, littérature, pédagogie, philosophie, traduction, etc. donnant lieu à deux tomes par numéro depuis 2019. DELLA est une revue semestrielle. Elle paraît deux fois l’an (en février et en Août). En cas de nécessité, elle peut se consacrer à la publication des numéros spéciaux. La revue peut aussi faire un appel à thématique définie.Item Restricted Matumizi ya Mbinu ya Utanzia na Uibuaji wa Maudhui Katika Tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani.(Kabale University, 2024) Mundu, Alamira PriscillaTasnifu hii inahusu Matumizi ya mbinu ya utanzia na uibuaji wa maudhui katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya mbinu ya utanzia katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa matatu. Lengo la kwanza lilikuwa ni kuchambua matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia teule. Lengo la pili lilikuwa ni kufananisha na kutofautisha sifa bainifu za kitanzia, na lengo la tatu lilikuwa ni kutathmini maudhui yanayoibuliwa na matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia hizo. Wango la utafiti huu ni jumla ya tamthilia za Pauline Kea na Kithaka wa Mberia ambazo idadi yake ni sita. Tamthilia hizi zimegawika katika makundi mawili. Kundi la kwanza linahusu tamthilia tano za Kithaka wa Mberia ambazo ni: Natala 1997,Mchezo wa Karata, 1997, Bara Jingine, 2001, Kifo Kisimani, 2001 na Maua kwenye Jua la Asubuhi 2004. Miongoni mwa tamthilia hizi tatu mtafiti aliteua tamthilia ya Kifo Kisimani. Kundi la pili ni tamthilia ya Pauline Kea ya ni Kigogo 2016. Sampuli ya utafiti ni tamthilia mbili za Kigogo na Kifo Kisimani. Mchakato uliotumika kupata Sampuli ya utafiti ni usampulishaji lengwa na usampulishaji tabakishi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia kifaacha orodha hakiki, zikachambuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti uliongozwa na nadharia ya uhalisia wa Kijamaa. Matokeo yanabainisha kuwa matukio halisi katika tamthilia teule ni pamoja na; utokeaji wa vifo, kuibuka kwa magonjwa katika jamii, kufungwa kwa wahusika. Hali kadhalika, sifa bainifu za kitanzia ni kama vile; mhusika nguli anayetoka katika tabaka la juu, migogoro, matukio yanayoamsha hisia za woga, huzuni na huruma na Mwisho mbaya wa mhusika nguli. Maudhui yaliyoibulliwa na matukio halisi ya kitanzia ni pamoja na, ukiukwaji wa haki za binadamu, uongozi mbaya, ukatili, umaskini, tamaa na ubinafsi. Tafiti zaidi zinaweza kufanywa kwa kuangalia vipengele vingine au mbinu nyingine. Mbinu zinazoweza kuchambuliwa ni pamoja na ujensi ubabe dume katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani, maudhui makuu katika tamthilia teule na mbinu nyinginezo katika tamthilia hizo. Pia utafiti unaweza kufanyika kwa kutumia nadharia nyingine kama vile nadharia ya ufeministi.Item Restricted Translation of Folktales from Runyankore-Rukiga into English:(Kabale University, 2024) Tumuheirwe, KizitoThis study aims at translation of Runyankore-Rukiga folktales into English, identifying cultural and linguistic challenges and suggesting strategies to aid cross-cultural translation. Five folktales have been translated with explanatory footnotes about the hard-to-translate and/ or untranslatable words and expressions. The researcher back-translated two of them to verify the validity of the translation. The study was qualitative in nature. It relied on data from both primary and secondary sources. The study showed that translation faces culture related challenges, given that the languages are culturally distinct. It also showed that meaningful, “speaking” personal names and literary devices such as euphemisms, proverbs and proverbial expressions, idioms and idiomatic expressions, ideophones and onomatopoeia, similes and metaphors are sources of problems in translation. Some strategies to resolve these challenges have also been suggested: firstly, employing footnotes to explain the hard-to-translate and untranslatable culture-bound and linguistic items and expressions; secondly, using the three proverb and proverbial translation principles proposed by Beekman & Callow (1974, p. 139); and adopting the principle that some devices remain untranslated and are retained in the target language (Kaindl, 1999, p. 275). In addition, the researcher used the methods: literal translation and free translation for euphemisms, as proposed by Wang (2020, pp. 1176 -1177); plus Baker’s (1992) taxonomy of four idiom translation strategies. Lastly, the five simile and metaphor translation strategies proposed by Larson (1984, p. 254) were applied. The study recommended, firstly, that the government invests in and puts more emphasis on translation work and studies of this nature; secondly, that translators ensure they fully understand the source and the target languages and cultures; lastly, that translation be introduced into the language syllabus at secondary school level.Item Restricted Translation of Folktales from Runyankore-Rukiga into English:(Kabale University, 2024) Tumuhairwe, Kizito.This study aims at translation of Runyankore-Rukiga folktales into English, identifying cultural and linguistic challenges and suggesting strategies to aid cross-cultural translation. Five folktales have been translated with explanatory footnotes about the hard-to-translate and/ or untranslatable words and expressions. The researcher back-translated two of them to verify the validity of the translation. The study was qualitative in nature. It relied on data from both primary and secondary sources. The study showed that translation faces culture related challenges, given that the languages are culturally distinct. It also showed that meaningful, “speaking” personal names and literary devices such as euphemisms, proverbs and proverbial expressions, idioms and idiomatic expressions, ideophones and onomatopoeia, similes and metaphors are sources of problems in translation. Some strategies to resolve these challenges have also been suggested: firstly, employing footnotes to explain the hard-to-translate and untranslatable culture-bound and linguistic items and expressions; secondly, using the three proverb and proverbial translation principles proposed by Beekman & Callow (1974, p. 139); and adopting the principle that some devices remain untranslated and are retained in the target language (Kaindl, 1999, p. 275). In addition, the researcher used the methods: literal translation and free translation for euphemisms, as proposed by Wang (2020, pp. 1176 -1177); plus Baker’s (1992) taxonomy of four idiom translation strategies. Lastly, the five simile and metaphor translation strategies proposed by Larson (1984, p. 254) were applied. The study recommended, firstly, that the government invests in and puts more emphasis on translation work and studies of this nature; secondly, that translators ensure they fully understand the source and the target languages and cultures; lastly, that translation be introduced into the language syllabus at secondary school level.Item Restricted Translation of Folktales from Runyankore-Rukiga into English: A Case Study of Challenges and Strategies.(Kabale University, 2024) Tumuhairwe, KizitoThis study aims at the translation of Runyankore-Rukiga folktales into English, identifying cultural and linguistic challenges and suggesting strategies to aid cross-cultural translation. Five folktales have been translated with explanatory footnotes about the hard-to-translate and/ or untranslatable words and expressions. The researcher back-translated two of them to verify the validity of the translation. The study was qualitative in nature. It relied on data from both primary and secondary sources. The study showed that translation faces culture-related challenges, given that the languages are culturally distinct. It also showed that meaningful, “speaking” personal names and literary devices such as euphemisms, proverbs and proverbial expressions, idioms and idiomatic expressions, ideophones, and onomatopoeia, similes, and metaphors are sources of problems in translation. Some strategies to resolve these challenges have also been suggested: firstly, employing footnotes to explain the hard-to-translate and untranslatable culture-bound and linguistic items and expressions; secondly, using the three proverb and proverbial translation principles proposed by Beekman & Callow (1974, p. 139); and adopting the principle that some devices remain untranslated and are retained in the target language (Kaindl, 1999, p. 275). In addition, the researcher used the methods: literal translation and free translation for euphemisms, as proposed by Wang (2020, pp. 1176 -1177); plus Baker’s (1992) taxonomy of four idiom translation strategies. Lastly, the five simile and metaphor translation strategies proposed by Larson (1984, p. 254) were applied. The study recommended, firstly, that the government invests in and puts more emphasis on translation work and studies of this nature; secondly, that translators ensure they fully understand the source and the target languages and cultures; lastly, that translation be introduced into the language syllabus at secondary school level.