Institute of Languages (INSTL)
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Institute of Languages (INSTL) by Subject "Mbinu"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Restricted Dhima ya Mbinu ya Ucheshi Katika Fasihi: Uchunguzi Kifani Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani.(Kabale University, 2024) Atwijukire, BeatriceUtafiti huu ulilenga kuchunguza dhima ya mbinu ya ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha mbinu za ucheshi zinazojitokeza katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani, kueleza ufanano na utofautianaji wa ujitokezaji wa ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani na kutathmini dhima ya ucheshi katika kujenga maudhui katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umtindo iliyoasisiwa na Leech (1969). Nadharia hii hushikilia kwamba kazi za fasihi haziwezi kueleweka bila lugha. Kwa hivyo, jinsi ilivyotumiwa na msanii kuumba kazi yake ni aula msingi kabisa kwa uelekeo wa nadharia hii. Wango la utafiti huu ni Diwani tatu za Euphrase Kezilahabi ambazo ni Kichomi (1974), Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Sababu ya kuteua Diwani hizi ni kuwa Kezilahabi ni mshairi maarufu katika historia na maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. Utafiti ulitumia usampulishaji nasibu tabakishi. Diwani za Kezilahabi zilitabakishwa kulingana na mwaka zilimochapishwa na zile zilizotungwa hivi karibuni ndizo zilizoteuliwa yaani Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Data zilikusanywa na kupangiliwa vizuri kulingana na mada kuu na ndogondogo ambazo zilibuniwa kutoka Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani kwa kuzingatia madhumuni mahususi ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba mbinu za ucheshi kama majina ya majazi, misemo, taswira za kuchekesha, tanakali sauti, uradidi, na utohozi zinajitokeza kwa namna mbalimbali katika Diwani hizi mbili. Kila moja ikichangia kwa namna yake katika kujenga maudhui na kuwasilisha malengo ya mwandishi. Pia ucheshi unathibitisha kuwa ni chombo muhimu katika fasihi, si tu kwa ajili ya burudani bali pia kwa ajili ya kufikisha ujumbe muhimu kwa jamii. Kwa mfano ucheshi huonesha matendo maovu ya viongozi, hali ya maisha ya watu katika jamii nakadhalika. Kwa njia hii, mashairi haya yanajenga maudhui yanayovutia na yenye kuleta mwanga juu ya masuala ya kijamii na kibinadamu kwa namna inayoeleweka na kukubalika na wasomaji. Utafiti ulipendekeza kwamba watafiti watakaofuata wa kazi za fasihi waendelee kuchunguza namna mbinu za ucheshi zinavyoweza kuendelezwa kwa ubunifu ili kuvutia wasomaji na kuwasilisha maudhui yenye thamani kwa jamii.Item Restricted Matumizi ya Mbinu ya Utanzia na Uibuaji wa Maudhui Katika Tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani.(Kabale University, 2024) Mundu, Alamira PriscillaTasnifu hii inahusu Matumizi ya mbinu ya utanzia na uibuaji wa maudhui katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya mbinu ya utanzia katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa matatu. Lengo la kwanza lilikuwa ni kuchambua matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia teule. Lengo la pili lilikuwa ni kufananisha na kutofautisha sifa bainifu za kitanzia, na lengo la tatu lilikuwa ni kutathmini maudhui yanayoibuliwa na matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia hizo. Wango la utafiti huu ni jumla ya tamthilia za Pauline Kea na Kithaka wa Mberia ambazo idadi yake ni sita. Tamthilia hizi zimegawika katika makundi mawili. Kundi la kwanza linahusu tamthilia tano za Kithaka wa Mberia ambazo ni: Natala 1997,Mchezo wa Karata, 1997, Bara Jingine, 2001, Kifo Kisimani, 2001 na Maua kwenye Jua la Asubuhi 2004. Miongoni mwa tamthilia hizi tatu mtafiti aliteua tamthilia ya Kifo Kisimani. Kundi la pili ni tamthilia ya Pauline Kea ya ni Kigogo 2016. Sampuli ya utafiti ni tamthilia mbili za Kigogo na Kifo Kisimani. Mchakato uliotumika kupata Sampuli ya utafiti ni usampulishaji lengwa na usampulishaji tabakishi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia kifaacha orodha hakiki, zikachambuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti uliongozwa na nadharia ya uhalisia wa Kijamaa. Matokeo yanabainisha kuwa matukio halisi katika tamthilia teule ni pamoja na; utokeaji wa vifo, kuibuka kwa magonjwa katika jamii, kufungwa kwa wahusika. Hali kadhalika, sifa bainifu za kitanzia ni kama vile; mhusika nguli anayetoka katika tabaka la juu, migogoro, matukio yanayoamsha hisia za woga, huzuni na huruma na Mwisho mbaya wa mhusika nguli. Maudhui yaliyoibulliwa na matukio halisi ya kitanzia ni pamoja na, ukiukwaji wa haki za binadamu, uongozi mbaya, ukatili, umaskini, tamaa na ubinafsi. Tafiti zaidi zinaweza kufanywa kwa kuangalia vipengele vingine au mbinu nyingine. Mbinu zinazoweza kuchambuliwa ni pamoja na ujensi ubabe dume katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani, maudhui makuu katika tamthilia teule na mbinu nyinginezo katika tamthilia hizo. Pia utafiti unaweza kufanyika kwa kutumia nadharia nyingine kama vile nadharia ya ufeministi.