Matumizi ya Mbinu ya Utanzia na Uibuaji wa Maudhui Katika Tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani.

dc.contributor.authorMundu, Alamira Priscilla
dc.date.accessioned2025-02-06T14:44:39Z
dc.date.available2025-02-06T14:44:39Z
dc.date.issued2024
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu Matumizi ya mbinu ya utanzia na uibuaji wa maudhui katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya mbinu ya utanzia katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa matatu. Lengo la kwanza lilikuwa ni kuchambua matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia teule. Lengo la pili lilikuwa ni kufananisha na kutofautisha sifa bainifu za kitanzia, na lengo la tatu lilikuwa ni kutathmini maudhui yanayoibuliwa na matukio halisi ya kitanzia katika tamthilia hizo. Wango la utafiti huu ni jumla ya tamthilia za Pauline Kea na Kithaka wa Mberia ambazo idadi yake ni sita. Tamthilia hizi zimegawika katika makundi mawili. Kundi la kwanza linahusu tamthilia tano za Kithaka wa Mberia ambazo ni: Natala 1997,Mchezo wa Karata, 1997, Bara Jingine, 2001, Kifo Kisimani, 2001 na Maua kwenye Jua la Asubuhi 2004. Miongoni mwa tamthilia hizi tatu mtafiti aliteua tamthilia ya Kifo Kisimani. Kundi la pili ni tamthilia ya Pauline Kea ya ni Kigogo 2016. Sampuli ya utafiti ni tamthilia mbili za Kigogo na Kifo Kisimani. Mchakato uliotumika kupata Sampuli ya utafiti ni usampulishaji lengwa na usampulishaji tabakishi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia kifaacha orodha hakiki, zikachambuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti uliongozwa na nadharia ya uhalisia wa Kijamaa. Matokeo yanabainisha kuwa matukio halisi katika tamthilia teule ni pamoja na; utokeaji wa vifo, kuibuka kwa magonjwa katika jamii, kufungwa kwa wahusika. Hali kadhalika, sifa bainifu za kitanzia ni kama vile; mhusika nguli anayetoka katika tabaka la juu, migogoro, matukio yanayoamsha hisia za woga, huzuni na huruma na Mwisho mbaya wa mhusika nguli. Maudhui yaliyoibulliwa na matukio halisi ya kitanzia ni pamoja na, ukiukwaji wa haki za binadamu, uongozi mbaya, ukatili, umaskini, tamaa na ubinafsi. Tafiti zaidi zinaweza kufanywa kwa kuangalia vipengele vingine au mbinu nyingine. Mbinu zinazoweza kuchambuliwa ni pamoja na ujensi ubabe dume katika tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani, maudhui makuu katika tamthilia teule na mbinu nyinginezo katika tamthilia hizo. Pia utafiti unaweza kufanyika kwa kutumia nadharia nyingine kama vile nadharia ya ufeministi.
dc.identifier.citationMundu, Alamira Priscilla (2024). Matumizi ya Mbinu ya Utanzia na Uibuaji wa Maudhui Katika Tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani. Kabale: Kabale University.
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/2880
dc.language.isoen
dc.publisherKabale University
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United Statesen
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/
dc.subjectMatumizi
dc.subjectMbinu
dc.subjectUtanzia
dc.subjectUibuaji
dc.subjectMaudhui
dc.subjectTamthilia
dc.subjectKigogo
dc.subjectKifo Kisimani
dc.titleMatumizi ya Mbinu ya Utanzia na Uibuaji wa Maudhui Katika Tamthilia ya Kigogo na Kifo Kisimani.
dc.typeThesis

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Mundu Alamira Priscilla-2024-MAK-Research Dissertation.pdf
Size:
1.72 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: