Dosari Za Kifonolojia Zinazojidhirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Katika Jamii Ya Wachiga: Uzingativu Wa Muktadha Wa Kujifunzia.

dc.contributor.authorTurigye, Rosemary
dc.date.accessioned2025-02-06T14:44:49Z
dc.date.available2025-02-06T14:44:49Z
dc.date.issued2024
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu dosari za kifonolojia zinazojitokeza miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Kichiga. Lengo lilikuwa kutalii ili kuona muktadha wa kijamii unavyoukilia ujitokezaji wa dosari hizo za kifonolojia. Kwa mahsusi kabisa, utafiti huu ulilenga kubainisha dosari za kifonolojia, kuelewa chanzo chake, kuzingatia muktadha wa kujifunza, na kutoa mapendekezo ya mikakati inayoweza kutumika kupunguza dosari hizo. Utafiti ulitumia sampuli ya watoa taarifa 94 waliogawanyika katika sehemu mbili, walimu 10 na wanafunzi 84. Mbinu za kukusanya data zilizotumika ni uandishi wa insha na hojaji. Hojaji zilitumika kwa walimu na wanafunzi wakati uandishi ulitumika kwa wajifunzaji lugha. Utafiti uliongozwa na Nadharia Uchanganuzi Makosa na Nadharia Elekezi hasa kwa mahsusi wake muhimili wa ingizo. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa dosari za udondoshaji, uchopekaji na ubadilishaji wa sauti zilibainika. Utafiti umebaini kuwa chanzo cha dosari hizo ni pamoja na uhamishaji, athari za lugha ya Kichiga, utamaduni wa Kichiga na ukakamaaji. Vilevile, imebainika kwamba, muktadha wa kijamii unachochea kwa kiasi kikubwa uibuzi wa dosari za kifonolojia kutokana na ukosefu wa uibuzi wa ingizo ndani ya mazingira miongoni mwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii. Muktadha wa kujifunzia uligunduliwa kuwa una athari kubwa kwa ujitokezaji wa dosari za kifonolojia, kwani wajifunzaji walikuwa wakipata changamoto kutokana na ukosefu wa mazoezi na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mazingira yao ya kila siku. Aidha, mikakati anuwai ilipendekezwa ili kupunguza dosari za kifonolojia, kuongeza mazoezi ya kusikiliza na kuzungumza Kiswahili, kuboresha vifaa vya kufundishia na kujifunzia, na kuanzisha programu za msaada kwa wajifunzaji wenye dosari za kifonolojia. Kwa kufanya hivyo, inatarajiwa kuwa dosari za kifonolojia zinaweza kupunguzwa na ujuzi wa lugha ya Kiswahili unaweza kuboreshwa miongoni mwa wajifunzaji katika jamii ya Kichiga.
dc.identifier.citationTurigye, Rosemary (2024). Dosari Za Kifonolojia Zinazojidhirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Katika Jamii Ya Wachiga: Uzingativu Wa Muktadha Wa Kujifunzia. Kabale: Kabale University.
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/2881
dc.language.isoen
dc.publisherKabale University
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United Statesen
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/
dc.subjectDosari
dc.subjectKifonolojia Zinazojidhirisha
dc.subjectMiongoni
dc.subjectWajifunzaji
dc.subjectKiswahili
dc.subjectWachiga
dc.subjectMuktadha
dc.subjectKujifunzia
dc.titleDosari Za Kifonolojia Zinazojidhirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Katika Jamii Ya Wachiga: Uzingativu Wa Muktadha Wa Kujifunzia.
dc.typeThesis

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Turigye Rosemary-2024-MAL-Research Dissertation.pdf
Size:
2.06 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: