Dhima ya Mbinu ya Ucheshi Katika Fasihi: Uchunguzi Kifani Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani.

dc.contributor.authorAtwijukire, Beatrice
dc.date.accessioned2025-02-06T14:45:00Z
dc.date.available2025-02-06T14:45:00Z
dc.date.issued2024
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuchunguza dhima ya mbinu ya ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha mbinu za ucheshi zinazojitokeza katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani, kueleza ufanano na utofautianaji wa ujitokezaji wa ucheshi katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani na kutathmini dhima ya ucheshi katika kujenga maudhui katika Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umtindo iliyoasisiwa na Leech (1969). Nadharia hii hushikilia kwamba kazi za fasihi haziwezi kueleweka bila lugha. Kwa hivyo, jinsi ilivyotumiwa na msanii kuumba kazi yake ni aula msingi kabisa kwa uelekeo wa nadharia hii. Wango la utafiti huu ni Diwani tatu za Euphrase Kezilahabi ambazo ni Kichomi (1974), Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Sababu ya kuteua Diwani hizi ni kuwa Kezilahabi ni mshairi maarufu katika historia na maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. Utafiti ulitumia usampulishaji nasibu tabakishi. Diwani za Kezilahabi zilitabakishwa kulingana na mwaka zilimochapishwa na zile zilizotungwa hivi karibuni ndizo zilizoteuliwa yaani Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008). Data zilikusanywa na kupangiliwa vizuri kulingana na mada kuu na ndogondogo ambazo zilibuniwa kutoka Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani kwa kuzingatia madhumuni mahususi ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba mbinu za ucheshi kama majina ya majazi, misemo, taswira za kuchekesha, tanakali sauti, uradidi, na utohozi zinajitokeza kwa namna mbalimbali katika Diwani hizi mbili. Kila moja ikichangia kwa namna yake katika kujenga maudhui na kuwasilisha malengo ya mwandishi. Pia ucheshi unathibitisha kuwa ni chombo muhimu katika fasihi, si tu kwa ajili ya burudani bali pia kwa ajili ya kufikisha ujumbe muhimu kwa jamii. Kwa mfano ucheshi huonesha matendo maovu ya viongozi, hali ya maisha ya watu katika jamii nakadhalika. Kwa njia hii, mashairi haya yanajenga maudhui yanayovutia na yenye kuleta mwanga juu ya masuala ya kijamii na kibinadamu kwa namna inayoeleweka na kukubalika na wasomaji. Utafiti ulipendekeza kwamba watafiti watakaofuata wa kazi za fasihi waendelee kuchunguza namna mbinu za ucheshi zinavyoweza kuendelezwa kwa ubunifu ili kuvutia wasomaji na kuwasilisha maudhui yenye thamani kwa jamii.
dc.identifier.citationAtwijukire, Beatrice (2024). Dhima ya Mbinu ya Ucheshi Katika Fasihi: Uchunguzi Kifani Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani. Kabale: Kabale University.
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/2882
dc.language.isoother
dc.publisherKabale University
dc.subjectDhima
dc.subjectMbinu
dc.subjectUcheshi
dc.subjectFasihi
dc.subjectUchunguzi
dc.subjectDiwani
dc.subjectDhifa
dc.subjectKaribu Ndani
dc.titleDhima ya Mbinu ya Ucheshi Katika Fasihi: Uchunguzi Kifani Diwani ya Dhifa na Karibu Ndani.
dc.typeThesis

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Atwijukire Beatrice-2024-MAK-Thesis.doc
Size:
8.47 MB
Format:
Microsoft Word
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: