Browsing by Author "Nuwamanya, Levinari"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Embargo Uhakiki Wa Mtindo Wa Lug Ha Ka Tika Riwaya Ya Ndoto Ya Almasi Na Ken Walibora.(Kabale University, 2022) Nuwamanya, LevinariMatini yoyote ya fasihi huhitaji kusomwa na kueleweka iii ipate kuwa na maana. Hata hivyo, kueleweka kwa matini hujitokeza ikiwa msomaji ataelewa mtindo uliotumika. Japo huu ndio ukweli, tafiti nyingi zilizofanywa hazijaangazia mtindo kama kipengele kinachojisimamia na tena maarufu katika kufafanua maudhui.Vipengele vya kimtindo pia vina ushirikiano na uhusiano mkubwa katika kupitisha ujumbe uliokusudiwa katika kazi ya kisanaa. Fauka ya hayo, matumizi mwafaka ya vipengele mbalimbali vya kimtindo huifanya kazi ya fasihi kuwa na mnato, mvuto na uzuri wa kipekee. Hata hivyo, matumizi mabaya ya mtindo hupelekea kazi ya kifasihi kukosa usanii na hata uzuri wake, yaani huwa chapwa na huathiri namna ujumbe unavyomfikia msomaji. Msanii yeyote anapokata shauri kuchagua vipengele fulani vya kisanaa sharti viweze kuvutia hadhira, kuchokonoa na kuathiri hisia zao. Mtindo unakuwa ni kigezo cha kupimia kufaulu au kutofaulu kwa msanii katika usanii wake. Mtunzi wa riwaya huhitaji weledi wa hali ya juu iii kuweza kufikia upeo wa ubunifu wake. Mapitio tangulizi ya maandishi yameonyesha kuwa hakuna utafiti uliofany wa kwa kina katika kubainisha mtindo kwenye riwaya ya Ndoto ya Almasi.