Browsing by Author "Musiimenta, Anita"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Restricted Hali ya Kiswahili Katika Shule za Upili Wilayani Ntungamo Nchini Uganda.(Kabale University, 2024) Musiimenta, AnitaKatika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaakwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa hawaoni umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, nchi ya Uganda inaweza kunufaika pakubwa sana hasa kiuchumi kutokana na lugha ya Kiswahili. Ni jambo la wazi kuwa uchumi duni hufanya nchi ikose kupata maendeleo ilhali uchumi imara hufanya nchi iwe na maendeleo. Nchi zenye nguvu kama vile Marekani na zile za Ulaya zimeweza kupata maendeleo makubwa kwa sababu ya kuwa na uchumi imara. Kwa hiyo, nchi mbalimbali huweka mikakati maalumu ya kuimarisha uchumi zao. Nchi huwa zinaimarisha uchumi zaokwa kuimarisha sekta za biashara, kilimo, viwanda, uvuvi na utalii. Halikadhalika, nchi nyingi hutenga kiasi kikubwa cha pesa katika bajeti zao za kila mwaka wa kifedha kwa ajili ya kuimarisha sekta mbalimbali zinazoimarisha uchumi. Nchi mbalimbali pia huendeleza sekta ya kibinafsi katika harakati zao za kuimarisha uchumi na kuondoa umaskini katika jamii. Kwa hiyo, watu binafsi huwa wanahamasishwa kuanzisha miradi mbalimbali na kubuni kazi kwa wananchi badala ya kusubiri serikali. Hata hivyo, nchini Uganda, wanasiasa hawajaona umuhimu wa lugha ya Kiswahili na nchi hii ni mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa hiyo, katika makala hii, mtafiti anaeleza jinsi Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa Waganda. Utafiti huu ulikusudia kujibu swali; Je, Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa yoyote kwa nchi ya Uganda? Katika kazi hii, mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Mtafiti aliendeleza utafiti katika Wilaya ya Bududa nchini Uganda. Wahojiwa walikuwa walimu katika shule za sekondari. Taarifa zilikusanywa kutoka kwa walimu 100. Baada ya taarifa kukusanywa, mtafiti alizichanganua data hizo na kubainisha hoja tofautitofauti. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa ulipelekea wananchi wa Uganda kuona umuhimu wa lugha ya Kiswahili na hivyo kuanza kuitetea badala ya kuipiga vita.