Nsimamukama, Mariseera2024-06-242024-06-242024Nsimamukama, Mariseera (2024). Uchanganuzi Wa Athari Za Kifonolojia Zinazojidhihirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Kama Lugha Ya Kigeni Katika Jamii Ya Wanyankore. Kabale: Kabale University.http://hdl.handle.net/20.500.12493/2113Mada kuu ya utafiti huu ilikuwa Uchanganuzi wa athari za kifonolojia zinazojidhihirisha miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika jamii ya Wanyankore. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza athari za kifonolojia zinazodhihirisha miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika jamii ya Wanyankore. Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ya watu sitini (60). Wanafunzi hamsini na walimu kumi kutoka kwa shule teule. Njia zilizotumiwa kukusanya data ni mahojiano kwa walimu wa Kiswahili na usimuliaji wa hadithi kwa wanafunzi wa Kiswahili. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi matatu na matokeo ya lengo la kwanza yalionyesha kwamba athari za Kifonolojia zinazojidhirisha miongoni mwa wajifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni katika jamii ya Wanyankore ni uchopekaji, ubadilishanaji wa fonimu na udoshaji herufi. Matokeo ya lengo la pili yalionyesha kuwa sababu kubwa ya kujitokeza kwa athari za Kifonolojia hizo ni mwingiliano wa lugha ya kwanza (Kinyankore) na lugha ya pili (Kiswahili). Matokeo ya lengo la tatu yalionyesha kwamba suluhisho kubwa la athari hizi ni kuwafundisha wanafunzi Kiswahili tangu utotoni ili wapate umilisi tosha. Mtafiti anapendekeza kwamba tafiti nyingine sifanywe kuhusu athari za kifonolojia Kwa kuangazia viwango vingine vya kiisimu ili suala hili lieleweke zaidi.enAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United Stateshttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/UchanganuziAthariKifonolojia ZinazojidhihirishaMiongoniWajifunzajiKiswahiliKama LughaKigeni KatikaWanyankoreUchanganuzi Wa Athari Za Kifonolojia Zinazojidhihirisha Miongoni Mwa Wajifunzaji Wa Kiswahili Kama Lugha Ya Kigeni Katika Jamii Ya Wanyankore.Thesis