Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.

dc.contributor.authorMasika, Doreen
dc.date.accessioned2023-03-06T06:33:31Z
dc.date.available2023-03-06T06:33:31Z
dc.date.issued2022
dc.description.abstractMradi huu wa tamthilia umepewa anwani ya " kiza cha mchana " kimaksudi. K wa kawaida kiza hujitokeza wakati wa usiku lakini siyo wakati wa mchana kwa hivyo kiza kikijitokeza mchana kuna maana kwamba kuna kitu ambacho hakiko sawa. Mtu yeyote azaliwapo huwa anatarajia mema na ufanisi katika maisha yake lakini baadhi ya watu duniani na katika nchi hii, matarajio yao hugeuka ndoto ya mchana yaani huishia yakiwa kinyume kabisa na matarajio ya watu hawa. Mradi wa tamthilia ya "kiza cha mchana" utadhihirisha wazi wazi jinsi baadhi ya watu wanakumbana na matatizo chungu nzima; tatizo baada yajingine mpaka wanapoanza kujichukia na kulaani siku walizozaliwa. Tamthilia hii itamtia mtu moyo ambaye anakumbana na matatizo katika maisha yake kwamba matatizo ni sehemu ya maisha ya binadamu na sio mwisho wa maisha ya binadamu, wakiyavumilia wakaendelea kujitahidi kadri ya uwezo wao huku wakimwomba Rabana, mwishowe watafanikiwa na hali yao kubadilika kabisa na kuanza kuishi kwa raha mustarehe. Mhusika mkuu, Matatizo ambaye ni fakiri atakumbana na matatizo mengi; moja baada ya jingine licha ya kuwa mchochole wa kupigiwa mfano. Matatizo analemewa na kuanza kujichukia na mwishowe anaokoka na baada ya muda mfupi anafanikiwa na kutajirika kutokana na bahati asiyoilalia wala kuiamkia. Watu kama hawa huishia kwa kujitia kitanzi baada ya kukumbana na mfululizo wa matatizo kama njia ya kuondokea matatizo haya na kuiacha familia yao katika dhiki kubwa. Kwa hivyo, mradi huu unapinga kabisa kuj itia kitanzi kama suluhisho la mfululizo wa matatizo bali kuwatia moyo na kuendelea kufukuza ndoto zao huku wakiimezea mate machungu hali yoyote ile wanayokumbana nayo mpaka watakapofaulu. Matatizo hapa amechorwa kama maskini, mvumilivu, ili kuwapa watu kama hawa mfano mzuri. Mradi wa tamthilia utapangwa katika vitendo vitatu na kila kitendo kitakuwa na maonyesho matatu. Kila kitendo kitakuwa na maudhui kuu linalozungumziwa humo ambalo linajitosheleza. Kila onyesho litakuwa na maudhui kuu pamoja na maudhui mengine madogo. Maudhui haya ya vitendo na maonyesho yatachangiana na kukamilishana na kufanya tamthilia nzima yenye wazo kuu la matatizo yaani anwani yenyewe ya mradi. Maudhui yatakayoshughulikiwa yatakuwa miongoni mwa utabaka, matatizo, uasherati, migogoro ya kifamilia, uvumilivu, ukengeushi, unafiki, mabadiliko, dini, baraka. vi Msanii wa mradi atatumia wahusika mbalimbali ambao ni pamoja na wahusika wakuu, wahusika wadogo, wahusika bapa, wahusika mviringo na wahusika wa kisaikolojia. Wahusika hawa watakuwa na mienendo ambayo ni pamoja na wavumilivu, wajibikaji, waaminifu, wakengeushi, washerati, wapole, werevu masomoni, washauri wema. Wahusika wakuu ndio watakaosheheni ujumbe muhimu na wahusika wadogo watawasaidia wahusika wakuu kukamilisha dhamira na maudhui ya msanii. Mazungumzo yataendelezwa miongoni mwa wahusika hawa ambapo nafsi ya kwanza umoja (ni ) na wingi ( tu ) zitatumika hasa kuendeleza mazungumzo baina ya wahusika. Nyimbo, majazi, taswira navyo vitatumika kuwasilisha ujumbe. Wahusika hawa watakuwa na maleba ambayo yataambatana sambamba na mandhari husika na wazo litakalokuwa likiendelezwa na wahusika hawa. Maleba yatakayotumiwa yatakuwa pamoja na magwanda, majoho ya kitabibu, majoho ya mapadre, ndala, veli. Maelekezo ya jukwaa yatatumiwa ipasavyo iii kuwaielekeza hadhira kutambua kwa urahisi maleba, miondoko na maingio ya wahusika na sifa zao. Maelekezo ya jukwaa yataandikwa kwa hati za mkazo na kuwekwa katika mabano. Maelekezo ya jukwaa haya pia yataonyesha wakati na mandhari ambapo vitushi vitatendeka. Mandhari haya yatakuwa pamoja na nyumbani, shambani, zahanatini. hospitalini kanisani.en_US
dc.identifier.citationMasika, Doreen (2022). Mradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''. Kabale:Kabale University.en_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12493/1072
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherKabale Universityen_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectMradien_US
dc.subjectKuandikaen_US
dc.subjectTamthiliaen_US
dc.subjectKiza Cha Mchanaen_US
dc.titleMradi wa Kuandika Tamthilia ya "Kiza Cha Mchana''.en_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Masika Doreen-KED-2022.pdf
Size:
283.22 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: