Mchango wa Fasihi Andishi ya Kiswahili Katika Kukuza Stadi za Uandishi Lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Upili Katika Munisipali ya Kabale Wilayani Kabale.
No Thumbnail Available
Date
2024
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kabale University
Abstract
Mada hii inahusisha mchango wa fasihi ya Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za upili. Fasihi andishi ni sehemu muhimu ya utamaduni na elimu, na inachangia pakubwa na uelewa wa wanafunzi.Mbinu za utafiti zilizotumiwa ni mbinu ya maktaba, mbinu ya hojaji, mahojiono, sampuli lengwa, mbinu za ukusanyaji wa data iliyotumika kutafuta data kwa shule za upili mbalimbali, kusoma kazi ya watafiti wengine nakusoma nyaraka mbalimbali katika maktaba ya chuo kikuu cha kabale.Fasi andishi inajumuisha Vitabu, Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi, Novela, Ushairi, na maandiko mengine ambayo yameandikwa kwa lugha ya Kiswahili.Inatoa mifano halisi ya matumizi sahihi ya lugha, muundo wa sentensi, na mbinu mbalimbali za uandishi. kwa wanafunzi wa shule za upili, kusoma fasihi andishi kunaweza kuwasaidia kuelewa vizuri kanuni za uandishi kama vile matumizi ya sarufi sahihi, mtindo wa kuandika, na jinsi ya kuwasilisha Mawazo yao kwa uwazi. Kwa hivyo, mchango wa fasihi andishi kati ka stadi za uandishi ni mkubwa sana. Inachangia si tu katika kuboresha ujuzi wa lugha bali pia inawasaidia wanafunzi kuwa wasomaji bora na waandishi wenye uwezo mkubwa katika jamii.
Description
Keywords
Mchango, Fasihi Andishi, Kiswahili, Kukuza Stadi, Uandishi Lugha, Wanafunzi, Shule, Upili, Munisipali, Wilayani Kabale
Citation
Kyasimire, Loyce (2024). Mchango wa Fasihi Andishi ya Kiswahili Katika Kukuza Stadi za Uandishi Lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Upili Katika Munisipali ya Kabale Wilayani Kabale. Kabale: Kabale University.