Makosa ya Upatanisho wa Kisarufi Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Katika Shule za Upili Wilayani Kasese.
No Thumbnail Available
Date
2024
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kabale University
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza makosa ya upatanisho wa kisarufi miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili wilayani Kasese. Utafiti huu ulijihusisha na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili katika mazingira ya lugha ya kwanza ya Kikonzo. Makosa ya upatanisho wa kisarufi yalibainishwa, kategoria za sababu za makosa ya upatanisho wa kisarufi pia yalibainishwa na hatua za kukabiliana na makosa hayo. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwepo kwa makosa ya upatanisho wa kisarufi katika kazi andishi na zungumshi za wanafunzi wa shule za upili wanaojifunza lugha ya Kiswahili hasa kutokana na harakati na jitihada za kujifunza. Athari za lugha ya kwanza pia zimejitokeza kama chanzo za makosa ya upatanisho wa kisarufi. Makosa hayo yanadhihirika katika vipengele vya ujuzi na uzalishaji wa matamko na maandishi.
Description
Keywords
Makosa, Upatanisho, Kisarufi, Ujifunzaji, Lugha, Kiswahili, Shule, Wilayani Kasese
Citation
Baluku, Joel (2024). Makosa ya Upatanisho wa Kisarufi Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Katika Shule za Upili Wilayani Kasese. Kabale: Kabale University.