Uchunguzi wa Sababu za Kuwapo Kwa Wanafunzi Wachache Wanaolichagua Somo la Kiswahili Katika Kiwango Cha “A” Nchini Uganda: Mfano wa Shule za Upili Wilayani Rukungiri.

No Thumbnail Available

Date

2024

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Kabale University

Abstract

Katika Tasnifu, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo kwa kila mwanafunzi unapofika, wanafunzi huwa na sababu za kimsingi zinazowafanya wapendelee masomo fulani na kuyakataa mengine. Kwa kawaida wanafunzi huwa hawalazimishwi kuchukua masomo fulani. Kila mwanafunzi huwa na uhuru wa kuchagua masomo anayoyapenda. Imebainika wazi kuwa nchini Uganda, wakati wa wanafunzi kupunguza idadi ya masomo unapofika, wengi wao huwa wanaacha somo la Kiswahili. Katika darasa la wanafunzi mia moja, ni wanafunzi kumi au kumi na watano tu ndio wanachukua Kiswahili. Hali hii inatisha sana hasa kwa wapenzi wa Kiswahili. Hivyo basi, mtafiti aliendeleza utafiti huu ili kueleza sababu zinazopelekea wanafunzi kufanya hivyo. Dhamira ya utafiti ni kueleza bayana kwa nini wanafunzi wengi nchini Uganda huwa hawachukui somo la Kiswahili katika kiwango cha “A”. Madhumuni ya utafiti huu ni kueleza mielekeo ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda dhidi ya ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili na Kupendekeza njia mbalimbali za kuondokana na sababu za kuwapo kwa wanafunzi wachache wanaolichagua somo la kiswahili katika kiwango cha “A” katika shule za upili wilayani Rukungiri. Katika kazi hii, mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Utafiti huu umeonyesha kuwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda huwa hawapendelei somo la Kiswahili kwa sababu zifuatazo: kuwepo na sera mbovu nchini kuhusu lugha ya Kiswahili; wanafunzi kutokuwa na msingi wa lugha ya Kiswahili; wanafunzi kuwa na fikra potovu kuwa Kiswahili ni lugha ya wezi; wanafunzi kufikiria kuwa Kiswahili ni somo linalofaa wenzao kutoka Kenya na Uganda; wanafunzi kufikiria kuwa lugha ya Kiswahili ni ngumu;

Description

Keywords

Uchunguzi, Sababu, Kuwapo, Wanafunzi Wachache, Wanaolichagua Somo, Kiswahili, Kiwango Nchini Uganda, Shule, Wilayani Rukungiri

Citation

Mpobwengye, Horeb (2024). Uchunguzi wa Sababu za Kuwapo Kwa Wanafunzi Wachache Wanaolichagua Somo la Kiswahili Katika Kiwango Cha “A” Nchini Uganda: Mfano wa Shule za Upili Wilayani Rukungiri. Kabale: Kabale University.